Featured Kitaifa

TFRA YAWEKA WAZI MAFANIKIO YAKE KIPINDI CHA MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA

Written by mzalendoeditor

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Bw. Joel Laurent akizungumza na waandishi wa habari  leo Machi 19,2025 jijini Dodoma kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Bw. Joel Laurent akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 19,2025 jijini Dodoma kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Na.Alex Sonna_DODOMA

KATIKA kipindi Cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita,Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imeanzisha Maabara ya kisasa ya mbolea.

Hayo yamesemwa leo Machi 19,2025 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA, Joel Laurent,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema kuwa Tanzania inakuwa nchi ya kwanza katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa na Maabara mahususi ya mbolea.

“Maabara hii inauwezo wa kupima sampuli za mbolea, udongo na tishu za mimea. Hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha udhibiti wa ubora wa mbolea nchini.”amesema Bw.Laurent

Aidha, amesema kuwa maabara hiyo inatarajiwa kutoa huduma kwa nchi jirani zinazotumia bandari za Tanzania, kama vile Malawi, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Burundi, na Rwanda.

Hata hivyo amesema kuwa  Kampuni ya ESSA Group ya Indonesia imeonesha nia ya kujenga kiwanda cha kuzalisha tani 1,000,000 za mbolea kwa mwaka unaotarajiwa kugharimu Dola za Marekani Bilioni 1.3 sawa na Sh.Trilioni 3.94.

“Uwekezaji huo unakusudia kuanza Mwaka 2029 na kiwanda kinatarajia kutoa ajira 4,500 za moja kwa moja wakati wa ujenzi, ajira 5,000 wakati wa uzalishaji pamoja na ajira zisizo za moja kwa moja 389,000.”amesema

About the author

mzalendoeditor