Featured Kitaifa

TUME KUONGEZA BVR VITUO VYENYE WATU WENGI DAR

Written by mzalendo
Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele akimkabidhi
kadi mpya ya Mpiga Kura Ndg. Abubakari Majuto mkazi wa Mzambarauni Kata ya
Gongola Mboto Dar es Salaam ambaye ni mlemavu wa viungo alijitokeza kujiandikisha
katika kituo cha Shule ya Msingi Mzambarauni leo Machi 18, 2025.
Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele akimkabidhi
kadi mpya ya Mpiga Kura Ndg. Abubakari Majuto mkazi wa Mzambarauni Kata ya
Gongola Mboto Dar es Salaam ambaye ni mlemavu wa viungo alijitokeza kujiandikisha
katika kituo cha Shule ya Msingi Mzambarauni leo Machi 18, 2025.

Wananchi wakiwa katika moja ya vituo Jijini Dar es Salaam kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. 

Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele leo Machi
18, 2025 ametembelea baadhi ya vituo vya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura Mkoani Dar es Salaam na kushuhudia mwenendo wa zoezi hilo katiuka
siku ya pili.

Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele leo Machi
18, 2025 ametembelea baadhi ya vituo vya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura Mkoani Dar es Salaam na kushuhudia mwenendo wa zoezi hilo katika
siku ya pili. 

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari, leo Machi 18, 2025, ametembelea na kukagua vituo vya kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, katika Jimbo la Temeke, lililopo Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari, leo Machi 18, 2025, ametembelea na kukagua vituo vya kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, katika Jimbo la Temeke, lililopo Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira leo tarehe 18 Machi, 2025 ametembela vituo mbalimbali vya kuandikisha Wapiga kura  Jimbo la Ilala Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuona zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linavyoendelea.

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira leo tarehe 18 Machi, 2025 ametembela vituo mbalimbali vya kuandikisha Wapiga kura  Jimbo la Ilala Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuona zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linavyoendelea.

Wananchi
wa Kata ya Kivule jijini Dar es Salaam wakiwa wamejitokeza kwa wingi
kujiandikisha na kuboiresha taarifa zao katika kituo cha Ukooni Kivule.

Na. Mwandishi Wetu 
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imesema
itaongeza mashine za BVR na watendaji katika vituo ambavyo vimebainika kuwa na
watu wengi ili kufanikisha uandikishaji na uborteshaji wa taarifa katika
Daftari la Kudumu lka Wapiga Kura mkoani Dar es Salaam.
 
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,
Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele ameyasema hayo leo Machi 18, 2025 katika
siku ya pili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati akikagua
vituo Mkoani Dar es Salaam.
 
“Leo katika siku ya pili ya zoezi
nimetembelea vituo vya uboreshaji na waliojitokeza wamekua wengi mmno kiasi
kwamba vifaa vinaonekana ni vichache, nimeagiza vifaa kwamba viongezwe na vituo
viongezwe ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo,” alisema Mhe. Jaji wa
Rufani Mwambegele.
 
Jaji Mwambegele akiwa katika Kituo cha
Lukooni Chanika Jijini Dar es Salaam alishuhudia uwepo wa wananchi wengi waliojitokeza
kwaajili ya kuboresha taarifa zao na kujiandikisha na kutoa maagizo ya
kuongezwa kwa mashine za BVR katika kituo hicho.
 
“Hapa Lukooni eneo la Chanika katika Wilaya
ya Ilala kulikua na kituo kimoja katika siku ya kwanza, lakini baada ya kubaini
kwamba watu wanakua ni wengi na wanatumia muda mrefu nikaagiza vifaa viongezwe
na leo nimepita bado nimeona BVR mbili hazitoshi kwahiyo nimeagiza ziongezwe
ili kuweza kukabiliana na changamoto hii,” aliongeza Jaji Mwambegele.
 
Aidha, Jaji Mwambegele amepongeza wananchi
wote waliojitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika siku
za mwanzo za zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu kwani kufanya hivyo
kunawezesha wao kukamilisha zoezi hilo ndani ya siku saba kama ilivyopangwa.
Nae afisa Mwandikishaji wa Jiji la Dar es
Salaam, Faraja Nakua amesema katika Majimbo matatu yaliyopo katika Halmashauriu
ya Jiji la Dar es Salaam yenye majimbo ya Ilala, Ukonga na Segerea zoezi
linakwenda vyema na wao wamejipanga kufanikisha zoezi hilo.
 
“Nizidi kuwahamasisha wananchi wa Majimbo ya
Ukonga, Ilala na Segerea Jijini Dar es Salaam kuendelea kujitokeza kwa wingi na
sisi tumejipanga kutekeleza zoezi hili kama ambavyo Tume imeagiza na vifaa
tulivyotakiwa kuongeza vipo tutavipeleka katika maeneo yote yenye changamoto,”
alisema Nakua.
 
Nae Atness Shayo mkazi wa Ukonga Mzambarauni
na Hassan Said Mmanga wa Chanika wamepongeza ujio wa zoezi hilo kwani
walipoteza kadi zao za mpiga Kura na sasa wameoata kadi zao mpya
zitakazoweawezesha kupiga Kura katika Uchaguzi Mkuu baadae mwaka huu.
 
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inataraji
kuandikisha Wapiga Kura wapya 643,420 mkoani Dar es Salaam ambapo jumla ya
vituo 1,757   vinatumika kwenye
uboreshaji kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo      96   
 katika vituo         1,661    vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka
2019/20.
 
Aidha Tume imejipanga kikamilifu kuhakikisha
wananchi wote wenye sifa za kuandikishwa wanaandikishwa kwani BVR zaidi ya
5,000 na watendaji wa kutosha wapo kwaajili ya utekelezaji wa zoezi hilo.
 
Tume imeshakamilisha uboreshaji wa Daftari
katika Mikoa 29. Kwa mujibu wa ratiba, leo Tume inaanza uboreshaji katika mzunguko
wa 13 ambao ni mzunguko wa mwisho wa uboreshaji wa Daftari. Mzunguko huu
unahusisha Mkoa wa Dar es Salaam pekee.
 
Kailima amesema kwa mkoa wa Dar es Salaam
Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 643,420 ikiwa ni sawa na ongezeko
la asilimia 18.7 ya wapiga kura 3,427,917 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura.
 
Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa
Dar es Salaam utakuwa na wapiga kura  
4,071,337 idadi ambayo inaweza kuongezeka kwa kuwa inawezekana wapo
watanzania ambao walikuwa na sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wakati wa
uboreshaji wa Daftari mwaka 2019/20, lakini kwa sababu moja au nyingine
hawakuweza kujiandikisha.
 
Zoezi la uboreshaji wa Daftari linahusu
kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18
na zaidi na watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka
2025, kutoa kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika
na kutoa fursa kwa wapiga kura walioandikishwa kurekebisha taarifa zao yakiwemo
majina na taarifa nyingine.
 
Uboreshaji wa Daftari pia unahusu kutoa fursa
kwa wapiga kura waliopo kwenye Daftari na ambao wamehama, waweze kuhamisha
taarifa zao kutoka kata au jimbo walipoandikishwa awali na kuondoa wapiga kura
waliopoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwa
ni pamoja na kuukana uraia wa Tanzania na kifo.

 

About the author

mzalendo