Featured Kitaifa

SERIKALI YATENGA BILIONI 25 KUTEKELEZA MRADI WA SLR UNAOSIMAMIWA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja ambaye pia ni Mwenyekiti wa kikao cha Kamati tendaji ya Usimamizi wa Mradi wa Urejeshwaji wa Mazingira na Hifadhi Endelevu ya Bayoanuai Tanzania (SLR-Tanzania) (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati hiyo Machi 15, 2025 Jijini Mbeya.

(NA MPIGAPICHA WETU)

Na Mwandishi Wetu,MBEYA

 

KATIBU Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kiasi cha Shilingi Bilioni 25 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania (SLR-Tanzania) ulioanza mwaka 2021-2025 katika Mikoa mitano na Halmashauri za Wilaya saba nchini.

Aidha kutokana na mwitikio chanya wa wananchi katika kutekeleza mradi huo, Serikali imekusudia kuongeza maeneo ya utekelezaji, katika Mikoa na Halmashauri nyingine nchini.

Mhandisi Luhemeja amesema hayo jana Jumamosi Machi 15, 2025 Jijini Mbeya wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati tendaji ya kitaifa ya usimamizi wa mradi huo kilichojadili shughuli mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo hadi kufikia sasa.

Luhemeja amesema tathimini iliyofanywa na Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, imeonesha wananchi wamefurahishwa na utekelezaji wa shughuli za mradi na hivyo Serikali imepanga kuhakikisha kuwa inaongeza wigo wa maeneo ya utekelezaji wake ili kuleta manufaa katika masuala ya uhifadhi wa mazingira nchni.

“Mwezi Oktoba mwaka huu tutafanya tathimini ya mradi na ili kuona uwezekano kupata maeneo mengi zaidi ya utekelezaji ili kutunza mazingira na pia kuwanufaisha jamii mbalimbali ambazo zimeweza kubuni miradi ya kijamii inayowaingia kipato kutokana na shughuli mbadala zinazoenda sambamba na uhifadhi endelevu wa mazingira” amesema Lihemeja.

Ameongeza kuwa mradi wa SLR ni mojawapo ya miradi ya mfano ambayo Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imekusudia kuianzisha katika maeneo mbalimbali nchini, ili kuisaidia jamii kuongeza hamasa ya uhifadhi wa mazingira na hivyo kuweza kutumia vyema fursa ya mabadiliko ya tabianchi kwa ajili ya kuibua miradi ya kijamii.

Amefafanua kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kujenga uwezo kwa jamii zinazotekeleza mradi huo ziweze kuhamasisha katika masuala ya uhifadhi wa  mazingira na kutumia fursa zilizopo kuweza kujiongeza kipato kupitia shughuli za uzalishaji mali.

“Tumeona Mkoa wa Katavi na Wilaya ya Mpimbwe wananchi wamehamasika kupanda miti na kuingia katika biashara ya kaboni na hivyo kujiongeza kipato…..Tumejipanga kuhakikisha fursa hizi pia zinaweza kuwanufaisha wananchi wa maeneo mbalimbali nchini” amesema Mhandisi Luhemeja.

Akitolea mfano, amesema kupitia mradi wa SLR wananchi wameweza kutumia mbinu za kisasa za uzalishaji mali ikiwemo kilimo rafiki kwa mazingira ambacho kimewazesha kuvuna kiasi kikubwa cha mazao kwa kutumia mbinu za kisasa ikiwemo mbegu bora na teknolojia ya umwagiliaji.

Aidha Luhemeja amezihimza jamii zilizonufaika na mradi huo kutumia vyema rasilimali zilizopo ili kuwa endelevu sambamba na kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha jamii kutunza na kuhifadhi mazingira kwani.

Kwa upande wake Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania (SLR), Dkt. Damas Mapunda amesema kwa mwaka 2025, mradi huo umetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 9.9 kwa ajili utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mradi.

“Mradi huo umepata hamasa kutoka kwa Viongozi wa ngazi mbalimbali pamoja na wananchi, hatua inayowezesha Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kuweza kufikia malengo iliyojiwekea ya urejeshwaji wa uoto wa asili katika maeneo mbalimbali nchini” amesema Dkt. Mapunda

Ameongeza kuwa hadi kufikia sasa mradi huo umefikia asilimia 67 ya utekelezaji wake na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kukamilisha mradi huo unakamilika kwa wakati na viwango vilivyokusudiwa.

Mradi wa SLR unafadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) kupitia Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na kusimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2021 na unatarajia kukamilika mwaka 2025 na ambapo jumla ya Mikoa 05, Halmashauri 07, Kata 18 na vijiji 54 zinatarajia kunufaika. Halmashauri hizo ni Iringa Vijijini, Mbeya, Wanging’ombe, Mbarali, Sumbawanga Vijijini, Tanganyika na Mpimbwe.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Usimamizi wa Mradi ya Mradi wa Urejeshwaji wa Mazingira na Hifadhi Endelevu ya Bayoanuai Tanzania (SLR-Tanzania) akizungumza na wajumbe wa kikao hicho kilichofanyika Machi 15, 2025 Jijini Mbeya.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Dkt. Samora Mshang’a akizungumza wakati wa kikao cha kamati tendaji ya usimamizi wa mradi wa urejeshwaji wa mazingira na hifadhi endelevu ya bayoanuai Tanzania kilichofanyika Machi 15, 2025 Jijini Mbeya. Katikati ni Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja.

Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Mradi wa Urejeshwaji wa Mazingira na Hifadhi Endelevu ya Bayoanuai Tanzania (SLR-Tanzania), Dkt. Damas Mapunda akifuatilia mjadala wakati wa kikao cha kikao cha Kamati Tendaji ya Usimamizi wa Mradi huo kilichofanyika Machi 15, 2025 Jijini Mbeya.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati Tendaji ya Usimamizi wa Mradi wa Urejeshwaji wa Mazingira na Hifadhi Endelevu ya Bayoanuai Tanzania (SLR-Tanzania) wakifuatilia mjadala wakati wa kikao cha kikao cha Kamati Tendaji ya Usimamizi wa Mradi huo kilichofanyika lMachi 15, 2025 Jijini Mbeya.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati tendaji ya usimamizi wa Mradi wa Urejeshwaji wa Mazingira na Hifadhi Endelevu ya Bayoanuai Tanzania (SLR-Tanzania) akizungumza na wajumbe mbalimbali muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao hicho Machi 15, 2025 Jijini Mbeya.

Mkurugenzi wa Huduma za Ugavi na Ununuzi Ofisi ya Makamu wa Rais ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati tendaji ya Usimamizi wa Mradi wa Urejeshwaji wa Mazingira na Hifadhi Endelevu ya Bayoanuai Tanzania (SLR-Tanzania), Bi. Juliana Mkalimoto akijitambulisha kwa wajumbe wa kikao hicho muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha kamati hiyo Machi 15, 2025 Jijini Mbeya.

Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais ambaye pia ni mjumbe wa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati tendaji ya Usimamizi wa Mradi wa Urejeshwaji wa Mazingira na Hifadhi Endelevu ya Bayoanuai Tanzania (SLR-Tanzania), Bi. Kemilembe Mutasa akifuatilia majadiliano ya kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Machi 15, 2025 Jijini Mbeya.

.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja ambaye pia ni Mwenyekiti wa kikao cha Kamati tendaji ya Usimamizi wa Mradi wa Urejeshwaji wa Mazingira na Hifadhi Endelevu ya Bayoanuai Tanzania (SLR-Tanzania) (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati hiyo Machi 15, 2025 Jijini Mbeya.

(NA MPIGAPICHA WETU)

About the author

mzalendoeditor