Featured Kitaifa

DKT. NCHEMBA ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UGANDA

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Uganda, Mhe Meja Jenerali Paul Simuli, alipotembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo Kampala nchini Uganda, baada ya kuhitimisha Mkutano wa 50 wa Benki ya Maendeleo Afrika Mashariki (EADB), ambapo aliwapongeza Mhe. Balozi wa Tanzania nchini humo na watumishi wa Ubalozi huo kwa kazi nzuri wanayofanya.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo Kampala nchini Uganda, baada ya kuhitimisha Mkutano wa 50 wa Benki ya Maendeleo Afrika Mashariki (EADB). Kushoto ni Balozi wa Tanzania Nchini Uganda, Mhe Meja Jenerali Paul Simuli.
 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Kampala-Uganda)

About the author

mzalendoeditor