Featured Kitaifa

EWURA YAWAKUMBUSHA WAFANYABIASHARA YA MAFUTA KUFUATA SHERIA,KANUNI NA TARATIBU

Written by mzalendoeditor

MENEJA wa Mamlaka  ya Udhibiti  wa Huduma za Nishati na Mafuta (EWURA) Kanda ya Ziwa  Bw.George Mhina,akizungumza wakati wa semina ya  wadau wa biashara ya mafuta iliyofanyika ukumbi wa ELCT-Bukoba, mkoani Kagera leo 13 Machi 2025. 

Na.Mwandishi Wetu-Bukoba

MENEJA wa Mamlaka  ya Udhibiti  wa Huduma za Nishati na Mafuta (EWURA) Kanda ya Ziwa  Bw.George Mhina amewakumbusha wadau kufuata sheria, kanuni, na taratibu katika kuendesha biashara ya mafuta hapa nchini wakati wa semina ya wadau iliyofanyika ukumbi wa ELCT-Bukoba, mkoani Kagera leo 13 Machi 2025.

Semina hiyo iliyolenga kutoa elimu kuhusu utaratibu wa kuomba leseni na udhibiti wa biashara ya mafuta na gesi ya kupikia, imejumuisha washiriki kutoka sekta binafsi na serikali mkoani Kagera.

“Wadau wa biashara ya Mafuta wanatakiwa kufuata kanuni,taratibu na Sheria  ambayo imekuwa ikitolewa na EWURA ili wasikutane na mkono wa sheria.”amesema Mhina

Hata hivyo ametakiwa kuhakikisha kuwa wanakuwa na akiba ya bidhaa za mafuta kila siku kwa ajili ya usambazaji kwa wateja wake kwa angalau siku tatu.
Vilevile,kuhakikisha ananunua bidhaa za mafuta kutoka kwa muuzaji mkubwa mwenye leseni ya EWURA na kutunza rekodi za manunuzi hayo kwa mujibu wa sheria na maagizo ya Mamlaka.
“Kuhakikisha kuna bango la bei linaloonesha bei za mafuta ambazo zimechapishwa. Bei zioneshwe
mahali pa wazi wakati wote,”amesema 
Kuhusu wajibu wa wamiliki wa leseni,amesema  wanatakiwa kuhakikisha kuwa anakagua na kusafisha matanki yake ya kuhifadhia mafuta angalau mara moja katika kipindi cha leseni na kuwasilisha ripoti kwa Mamlaka.
Amesema kuwa Mamlaka kupitia ofisi zake za Kanda imekuwa ikiweka jitihada katika kuhakikisha vituo vyote vinakidhi vigezo wakati wote kwa kuhakikisha kuwa inafanya kaguzi za mara kwa mara;
Pia,Mamlaka itaendelea kuhimiza uwekezaji wa vituo vya mafuta maeneo ya vijijini ili kusogeza huduma.

Washiriki wameishukuru EWURA kwa mafunzo hayo ambayo yamewapa fursa ya kuwasilisha kero na ushauri kwa Mamlaka huku wakiomba mafunzo ya aina hiyo kuwa endelevu.

 

About the author

mzalendoeditor