Featured Kitaifa

EWURA YAUNGA MKONO MKAKATI NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Written by mzalendoeditor

   

Na.Mwandishi Wetu-ARUSHA

MAMLAKA  ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema inaunga Mkono Jitihada za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,katika  kampeni ya matumizi sahihi ya nishati safi na salama kwa kuweka mazingira rahisi ya utoaji vibali kwa wawekezaji nchini.

Ofisi Mkuu,Uchambuzi wa Hesabu na Fedha na Mwenyekiti wa Wanawake TUGHE,Tawi la EWURA Bi.Herith Kasilima,ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la EWURA wakati wa maonesho ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kitaifa yalifanyika jijini Arusha.

Alisema katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani,wamekuwa chachu katika kuhamasisha matumizi sahihi na salama ya nishati ya kupikia na kuwataka wawekezaji wa nishati kuchangamkia fursa hiyo.

“EWURA imejipanga kuhamasisha wanawake wanatumia nishati safi ya kupikia kwa kutoa elimu kwa umma hususani wanawake ambao ndio watumiaji wakubwa wa nishati hiyo”amesema Bi.Kasilima

Aidha amesema kuwa EWURA inahamasisha wawekezaji wa Nishati kuwekeza nishati ya umeme ama gesi ya kupikia (LPG) katika maeneo ya umma baada ya kurahisisha utoaji vibali,hatua ambayo itasaidia wananchi kupata huduma hiyo na kuondokana na athari zinazotokana na matumizi ya kuni.

Naye,Mhandisi Mkuu wa umeme EWURA,Mwanamkuu Kanizio,amesema kuwa EWURA wameadhimisha siku hiyo kwa kutoa elimu na kuhamasisha makundi ya wanawake ili kuelewa umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia.

About the author

mzalendoeditor