Featured Kitaifa

WAFANYAKAZI WANAWAKE BARRICK WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUSAIDIA JAMII

Written by mzalendoeditor
Wafanyakazi wanawake wa kampuni ya Barrick nchini na wakandarasi wake wameshiriki maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa kujikita kutoa msaada kwenye jamii sambamba na kujitolea muda wao kusaidia shughuli za kijamii ambapo baadhi yao wameshiriki maadhimisho ya kitaifa yaliyofanyika katika jiji la Arusha.
 
Wanawake kutoka mgodi wa Barrick Bulyanhulu wametembelea hospitali ya rufaa ya ya wilaya Nyang’hwale na Kituo cha afya cha Khalumwa Mkoani Geita na kukabidhi vifaa mbalimbali vya usafi na vya kusaidia wagonjwa wanaopata huduma za kiafya katika sehemu hizo.
 
Akiongea wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa hivyo, Afisa Uhusiano wa Jamii Mwandamizi wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo amesema katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu 2025, pamoja na kampuni kuwa na programu mbalimbali za ndani pia imeandaa programu za kusaidia jamii.
 
Akiongea na uongozi wa Hospitali hiyo, Afisa Uhusiano kutoka Mgodi wa Barrick Bulaynhulu Zuwena Senkondo, amesema katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu 2025, pamoja na kampuni kuwa na programu mbalimbali za ndani pia imeandaa programu za kusaidia jamii.
 
Amesema Barrick imekuwa ikitoa kipaumbele kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha sekta ya afya nchini ambapo kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii imeweza kujenga vituo vya afya katika maeneo yanaozunguka migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara.
 
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Nyang’wale Dkt., Zakhia Abdallah , ameishukuru Barrick kwa msaada huo sambamba na baadhi ya wafanyakazi wake kujitolea muda wao kutembelea hospitali na kutembelea wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo ikiwemo Wanawake waliolazwa katika wodi ya wazazi.
 
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nyang’wale Octavianus Rweyendera, amewapongeza Wanawake wa Barrick kwa kutumia maadhimisho ya siku yao kusaidia wenye mahitaji katika jamii sambamba na kutenga muda wao kuwatembelea na kuwapatia faraja.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Barrick walioshiriki maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na wenye mahitaji maalum Dkt. Dorothy Gwajima katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake dunia kitaifa yaliyofanyika katika jiji la Arusha.
Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu na wakandarasi wake katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambapo wamekabidhi vifaa mbalimbali hospitali ya hospitali ya rufaa ya wilaya Nyang’hwale na Kituo cha afya cha Khalumwa Mkoani Geita

About the author

mzalendoeditor