Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA),Bi.Subira Kaswaga,akimkabidhi vifaa tiba na mahitaji muhimu kwa ajili ya wajawazito ,Ofisa Ustawi wa Jamii wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Tegemea Ngulwa,walipoenda kutoa msaada katika Hospitali hiyo,leo Machi 8,2025 jijini Dodoma.

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA),Bi.Subira Kaswaga,akimkabidhi vifaa tiba na mahitaji muhimu kwa ajili ya wajawazito ,Ofisa Ustawi wa Jamii wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Tegemea Ngulwa,walipoenda kutoa msaada katika Hospitali hiyo,leo Machi 8,2025 jijini Dodoma.



Wanawake Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoa msaada wa vifaa tiba na mahitaji muhimu kwa ajili ya wajawazito,katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.


Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA),Bi.Subira Kaswaga,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi vifaa tiba na mahitaji muhimu kwa ajili ya wajawazito katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Ofisa Ustawi wa Jamii wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Tegemea Ngulwa,akitoa shukrani kwa Wanawake wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kwa kuwakabidhi vifaa tiba na mahitaji muhimu kwa ajili ya wajawazito katika Hospitali hiyo ,leo Machi 8,2025 jijini Dodoma.







Picha katika matukio mbalimbali
Na.Alex Sonna-DODOMA
KATIKA kuadhimisha siku ya wanawake duniani, Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) Wanawake wametoa vifaa tiba na mahitaji muhimu kwa ajili ya wajawazito katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ili kuonesha thamani ya mwanamke kwa jamii.
Akizungumza leo Machi 8,2025 jijini Dodoma baada ya kukabidhi msaada huo, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Bi.Subira Kaswaga, alisema mamlaka hiyo inatambua na kuthamini wanawake na umuhimu wao kwa jamii jambo ambalo limewasukuma kutoa msaada huo.
Bi.amesema kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikirahisisha utendaji kazi wa serikali kupitia Tehama na wamekuwa wakishirikiana na Wizara ya Afya kutengeneza mifumo mbalimbali ili kuwarahisishia wagonjwa kupata huduma za kiafya.
“Mamlaka imerahisisha wananchi kupata huduma mahali walipo, katika kuhakikisha mamlaka inaleta haki na usawa katika utoaji huduma inatengeneza mifumo ya kuhakikisha kunakuwapo na haki na usawa bila kujali jinsia, kama mnavyoona kauli mbiu mwaka huu inasisitiza haki usawa na uwezeshaji na kupitia Tehama inatoa fursa kwa wanawake kujishughulisha na shughuli mbalimbali za ujasiriamali,”amesema
Naye, Ofisa Ustawi wa Jamii wa Hospitali hiyo, Tegemea Ngulwa, ameishukuru mamlaka hiyo kwa msaada huo kwa kuwa itasaidia wenye uhitaji na kutoa wito kwa taasisi zingine kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wagonjwa.