Featured Kitaifa

TUTOKOMEZE UKATILI WA KIJINSIA MAENEO YA UMMA

Written by mzalendoeditor
Maafisa mbalimbali kutoka Wizara ya
Maendeleo ya jamii wakitembelea soko kuu la Arusha kukagua dawati la kutokomeza ukatili linavyo fanya kazi
Wajumbe wa dawati la kutokomeza ukatili wa kijinsia Soko Kuu Arusha
Mkuu wa Soko Kuu na Katibu wa Dawati la Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia, Soko Kuu Arusha, John Francis Haule

***

Dawati la kutokomeza ukatili wa kijinsia katika Soko Kuu la Arusha limeendesha semina kwa wafanyabiashara sokoni hapa kwa lengo la kutoa elimu kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Katibu wa dawati hilo, Ndugu John Francis Haule, amesema kuwa dawati hili limeanzishwa kwa mujibu wa sheria na muongozo wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Malum, kwa lengo la kusaidia kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo ya umma.

“Leo tumeamua kuwafikia wafanyabiashara kwa kuwapa elimu ya umuhimu wa kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika eneo hili la umma”, amesema.

MAJUKUMU YA DAWATI LA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA ENEO LA UMMA

  1. Kutoa elimu juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
  2. Kushughulikia na kuwasaidia wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
  3. Kutoa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia.
  4. Kutunza kumbukumbu za wahanga wa ukatili wa kijinsia.
  5. Kuhamasisha jamii kutoa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia.

FAIDA ZA UWEPO WA DAWATI LA JINSIA KATIKA SOKO KUU ARUSHA

Dawati hili limesaidia sana kupunguza vitendo vya ukatili hasa matusi yanayohusiana na jinsia na ugomvi sokoni. Uelewa kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia umeongezeka sana kutokana na elimu inayotolewa mara kwa mara na wajumbe wa dawati. Hata dawati la jinsia la Jeshi la Polisi linakuja mara kwa mara kutoa elimu sokoni.

WAJUMBE WA DAWATI LA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA NAO WANENA

Akiwa katika semina, Bi. Juliet Laizier, mjumbe wa dawati la kutokomeza ukatili wa kijinsia, amesema:
“Kiukweli, dawati hili tangu lianzishwe hapa Soko Kuu limekuwa msaada mkubwa sana kwa sisi wafanyabiashara na hata wateja wanaokuja kufanya manunuzi. Elimu tunayoipata kupitia dawati hili inaongeza uelewa mkubwa kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia na madhara yake.”

 Bi. Laizier amesisitiza kwamba serikali inapaswa kuendelea kutoa msukumo kwa madawati haya katika maeneo ya umma, kwani ni muhimu sana katika kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia, hasa kwa wanawake na wasichana.

Naye,  Malya, ambaye ni Mwenyekiti wa Dawati la Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia, amesema kuwa utoaji elimu kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia sokoni ni jambo endelevu na litazidi kuendelea.

CHANGAMOTO ZA KUTOKOMEZA UKATILI KATIKA JAMII

Mila na desturi zinazozungumziwa kama kandamizi zinakuwa kikwazo katika kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia. Usiri katika jamii ni changamoto kubwa; vitendo hivi vinapojitokeza katika ngazi za jamii, inakuwa vigumu kuviweka wazi, jambo linalosababisha kutokuwepo kwa takwimu sahihi za vitendo vya ukatili wa kijinsia.


IMEANDALIWA NA:
John Francis Haule,
Mkuu wa Soko Kuu na Katibu wa Dawati la Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia, Soko Kuu Arusha
Simu: 0756717987 au 0711993907

About the author

mzalendoeditor