Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Wazee, na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu yaliyofanyika Mkoani Shinyanga leo, Machi 1, 2025
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Wazee, na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma, amewataka wanaume kuwa mstari wa mbele katika kuwalinda wanawake na watoto badala ya kuwa chanzo cha vikwazo.
Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu yaliyofanyika Mkoani Shinyanga leo, Machi 1, 2025, Mhe. Riziki ameweka wazi kuwa jamii inapaswa kushirikiana kwa pamoja ili kuimarisha haki, usawa, na uwekezaji, akisisitiza kuwa wanaume wanahitaji kuchukua jukumu kubwa la kuwalinda wanawake, watoto, na watu wenye ulemavu.
Maadhimisho hayo yameandaliwa na Shujaa Wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali yakiongozwa na kauli mbiu “Wanawake na Wasichana 2025, Tuimarishe Haki, Usawa na Uwekezaji”.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Wazee, na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma
“Tuendelee kupinga ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto. Wenye silaha za kufanyia ukatili ni wanaume, wenye silaha za ubakaji na ulawiti ni wanaume, naomba akina baba silaha zihifadhini vizuri, zitumike vizuri, pahala sahihi kwa watu sahihi, zisitumike kwa watoto wetu… zisionekane hovyo”,amesema Mhe. Riziki.
Aidha, Mhe. Riziki ametoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi ujao wa 2025, akisema kwamba wanawake wanapaswa kujiandaa kushiriki kwa wingi ili kuungana na viongozi wanaume katika kuboresha maendeleo ya taifa.
Amewashauri wanaume kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono mgombea mwanamke ili kuongeza uwakilishi wa wanawake katika uongozi, akisema “Wanawake wanapokuwa katika uongozi, huongeza mchango wa uchumi wa familia na jamii nzima.”
Mhe. Riziki pia amewapongeza wanawake wenye ulemavu kwa bidii na juhudi zao katika kuchangia maendeleo ya jamii, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali kuhakikisha kundi hilo linapata nafasi sawa katika sekta zote.
“Siku ya Wanawake Duniani ni fursa ya kutambua mchango wa wanawake wote, wakiwemo wenye ulemavu, katika maendeleo ya taifa. Ni jukumu letu kuhakikisha wanapata haki zao na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kiuchumi,” amesema Mhe. Riziki.
Amesema wanawake wenye ulemavu wanastahili pongezi kwa mchango wao katika jamii licha ya changamoto wanazokutana nazo, na kusema, “Siku ya Wanawake Duniani ni alama muhimu ya kutambua mchango wa wanawake wote, bila kujali hali zao. Tunapaswa kuhakikisha kuwa wanawake wenye ulemavu wanapata nafasi sawa katika elimu, ajira, na uongozi, ili wawe sehemu ya maendeleo ya nchi.”
Aidha, ameongeza kuwa serikali inaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha huduma za jamii kwa wanawake wote, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa elimu, huduma za afya, na maji safi, ili kuhakikisha wanapata mazingira bora ya maisha.
Akisoma risala, Katibu wa Idara ya Wenye Ulemavu SMAUJATA Taifa, Imani Axwesso, amebainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake wenye ulemavu, ikiwemo ukosefu wa ajira, mitaji ya biashara, mikopo, na nafasi za uongozi.
“Jamii inapaswa kuhakikisha kuwa wanawake wenye ulemavu wanashirikishwa kikamilifu katika nafasi za kimaendeleo ili waweze kujitegemea na kushiriki katika maamuzi ya uongozi,” amesema Axwesso.
Katibu wa Idara ya Wenye Ulemavu SMAUJATA Taifa, Imani Axwesso
Amesema changamoto zingine zinazowakabili wanawake wenye ulemavu, kama vile ukatili wa kijinsia, unyanyapaa, na ubaguzi katika jamii.
Aidha, amehimiza serikali na wadau wa maendeleo kuweka mikakati madhubuti ya kuwawezesha kiuchumi, na kuhakikisha wanapata huduma bora za elimu na afya.
Kwa upande mwingine, amehamasisha umuhimu wa malezi bora kwa watoto, hasa akijikita katika kutoa ushauri kwa wazazi na walezi kuwaepusha watoto na mazingira hatarishi, kama vile kuwalaza na wageni, ili kuepuka ukatili wa kijinsia.
“Kila kundi linapaswa kulindwa. Tuache ukatili wa kijinsia. Tunawapongeza SMAUJATA kwa jitihada zao za kupambana na ukatili wa kijinsia,” ameongeza Mhe. Riziki.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu amekiri juhudi za serikali katika kuboresha hali ya maisha kwa watu wenye ulemavu, hasa wanawake na watoto, kupitia mikopo na ajira.
Vilevile, amesema kuwa haki za watu wenye ulemavu zitazidi kuimarishwa na serikali itaendelea kutekeleza sheria na taratibu zinazolinda haki zao.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, amesema kuwa serikali na wadau wameendelea kushirikiana katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia, na ameelezea matumaini kuwa vita dhidi ya ukatili wa kijinsia itashinda, akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kupigania haki za wanawake na watoto.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Christina Mzava, ameelezea mfano bora wa Rais Samia Suluhu, ambaye anapigania haki za wanawake na wanawake wenye ulemavu.
“Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi, wanawake na watu wenye ulemavu, tusikubali kubaki nyuma. Tuchukue fomu na tushiriki katika nafasi za uongozi ili kuwa na sauti katika ngazi za maamuzi”,amesema.
Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa, Sospeter Mosewe Bulugu.
Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa, Sospeter Mosewe Bulugu, amewakumbusha wanaume kuacha kunyanyasa wanawake na kuhakikisha wanawake wanapata usalama, huku akisisitiza umuhimu wa kushirikisha wanawake wenye ulemavu katika masuala ya uongozi.
Amesema kuwa SMAUJATA ni jumuiya ya kijamii inayolenga kuchochea mabadiliko chanya na kuleta maendeleo endelevu kijamii na kiuchumi na ilianzishwa ili kuchochea shughuli za maendeleo na ustawi wa jamii, huku akieleza kuwa ilizinduliwa rasmi na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, mnamo Juni 16, 2022.
“Dira ya SMAUJATA ni kuwa na taifa lenye kizazi huru chenye haki na usawa, kitakachoweza kujitegemea na kuzitambua fursa, na kutumia ujuzi, maarifa, na vipaji katika kujenga jamii yenye maendeleo endelevu,” amesema Bulugu.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Wazee, na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu yaliyofanyika Mkoani Shinyanga leo, Machi 1, 2025 – Picha na Malunde
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Wazee, na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Wazee, na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Wazee, na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga
Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa, Sospeter Mosewe Bulugu akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga
Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga , Nabila Kisendi akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga
Katibu wa SMAUJATA Kanda ya Ziwa, Daniel Kapaya akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu Mkoani Shinyanga