Featured Kitaifa

TUME YATOA NENO KWA WAENDESHA VIFAA VYA BVR TANGA NA PWANI

Written by mzalendo
Na Mwandishi wetu, Tanga
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewataka waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki kutoa huduma bora kwa wananchi watakaojitokeza katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotaraji kuanza Februari 13 hadi 19, 2025 katika mikoa ya Tanga na Pwani.
 
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taiofa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele wakati alipotembelea mafunzo ya siku mbili ya waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki katika Halmashauri za Jiji la Tanga, Mji wa Korogwe pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe vijijini.
 
“Ninawasihi
muwahudumie wateja wenu kwa umahiri na unyenyekevu, msiwe na hasira kwani
miongoni mwa wateja mtakao kuwa mnawashughulikia wengine ni wavijijini na wengine
ni wamjini hivyo kila mtu anauelewa wake,” alisema Jaji Mwambegele.
 
Jaji wa
Rufaa Mwambegele amesema ni jukumulao kuwaelishisha juu ya nini cha kufanya na wakawaeleze
kwa upole na si kuwawakali bali kuwasaidia kuwaelekeza kwa unyenyekevu ili
zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura liweze kufanikiwa vyema kama ilivyo
kusudiwa.
 
Aidha,
akizungumza na washiriki hao akiwa Jijini Tanga, Jaji Mwambegele amewataka washiriki
hao kuwa waadilifu na kufanya kazi hiyo muhumu kwa taifa kwa moyo na kujituma.
 
Amewataka
pia kutunza vifaa vyote watakavyo kabidhiwa wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo
ili vifaa hivyo vilivyonunuliwa kwa gharama kubwa vikaweze kutumika katika maeneo
mengine pindi vikitunzwa vyema.
 
Uboreshaji
wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika mkoani Tanga na Pwani kwa siku
saba kuanzia tarehe 13 hadi 19 Februari, 2025 ambapo wapiga kura wapya 431,016
wanatarajiwa kuandikishwa na zoezi hilo litakapokamilika mikoa hiyo itakuwa na
wapiga kura 2,727,318 sawa na ongezeko la asilimia 18.7 ya wapiga kura
2,296,302 waliopo kwenye daftari katika mikoa hiyo.
 
Mkoa
wa Tanga zoezi la Uboreshaji litafanyika kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga,
Halmashauri za Miji ya Handeni na Korogwe na Halmashauri za Wilaya ya Kilindi,
Lushoto na Muheza na vituo vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa Saa 12:00
jioni kila siku kwa siku saba.
 
Tume
imeshakamilisha zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura  kwenye mikoa 27  ya Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera,
Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Manyara, Dodoma, Singida, Mjini Magharibi,
Kusini Unguja, Kaskazini Unguja, Kusini Pemba, Kaskazini Pemba, Arusha,
Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Rukwa, Songwe, Njombe, Ruvuma, Lindi na Mtwara. 
Mwenyekiti wa Tume, Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambege akiteta jambo na afisa Mwandikishaji Msaidizi Jimbo la Tanga mjini Bi. Mwanaidi Nondo. 

 

 

Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele leo
Februari 11,2025 ametembelea na kuzungumza na washiriki wa mafunzo ya siku
mbili ya waandishi wasaidizi na waendesha
vifaa vya bayometriki katika Halmashauri ya jiji la Tanga Mkoani Tanga. Zoezi la Uboreshaji
Mkoani humo linataraji kuanza Februari 13 hadi 19 mwaka huu. 

 

 

 

Washiriki wa mafunzo wakisikiliza neno kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume.

Washiriki wa mafunzo kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe  wakisikiliza neno kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume

Watoa mada wakati wa mafunzo Halmashauri ya Mji wa Korogwe wakiendelea na utoaji mada.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele leo Februari 11,2025 ametembelea na kuzungumza na washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya waandishi wasaidizi na waendesha  vifaa vya bayometriki katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe vijijini Mkoani Tanga. Zoezi la Uboreshaji Mkoani humo linataraji kuanza Februari 13 hadi 19 mwaka huu. 

 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele leo Februari 11,2025 ametembelea na kuzungumza na washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya waandishi wasaidizi na waendesha  vifaa vya bayometriki katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe vijijini Mkoani Tanga. Zoezi la Uboreshaji Mkoani humo linataraji kuanza Februari 13 hadi 19 mwaka huu. 

 

About the author

mzalendo