Featured Kitaifa

RIDHIWANI AITAKA JAMII KUONA UMUHIMU WA WANAWAKE NA WASICHANA KUINGIA KWENYE STEM

Written by mzalendoeditor
WAZIRI  wa Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe.Ridhiwani Kikwete,akizungumza wakati wa  kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi hafla iliyofanyika  leo Februari 11,2025 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma,wakati akimwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.
NAIBU  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia masuala ya Elimu Dkt. Charles Wilson Mahera,akizungumza wakati wa  kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi hafla iliyofanyika  leo Februari 11,2025 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia Sayansi na Elimu ya Juu Prof. Daniel Mushi ,akizungumza wakati wa  kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi hafla iliyofanyika  leo Februari 11,2025 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.
SEHEMU ya Wanafunzi wakimsikiliza Waziri   wa Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe.Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa  kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi hafla iliyofanyika  leo Februari 11,2025 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma,wakati akimwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.

WAZIRI  wa Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe.Ridhiwani Kikwete,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza kwenye   kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi hafla iliyofanyika  leo Februari 11,2025 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma,wakati akimwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.

Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI  wa Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete ameitaka jamii kuona  umuhimu wa kuhamasisha wanawake na wasichana kujiingiza katika fani za sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) ili kundi hilo liendelee kutoa mchango mkubwa kwa Taifa katika kutatua changamoto zilizopo katika jamii hapa nchini.
Mhe.Ridhiwani ameyasema hayo  ,wakati akimwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Na Wasichana katika Sayansi tukio lililofanyika leo Februari 11,2025 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.
Amesema kwa mujibu wa sensa ya watu na Makazi ya 2022 kundi la wanawake na wasichana ni asilimia 51.3  na kwamba kiwango Cha kundi hilo kinachoshiriki katika nyanja hizo ni asilimia 33 pekee.
“Hapa nchini Tanzania ,kiwango Cha kundi hilo kinachoashiria kazi za Sayansi Teknolojia na Hisabati kinakadiriwa kufikia asilimia 36.”amesema Mhe.Kikwete
Mhe.Ridhiwani amesema  kutokana na ushiriki wao mdogo nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania zinatekeleza juhufi zake zinazolenga kuweka mazingira wezeshi ya kummotisha msichana na mwanamke .
 “Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuhakikisha usawa wa kijinsia katika sekta hizi, ikiwa ni pamoja na kutoa fursa za elimu na mafunzo kwa wanawake na wasichana.”amesema 
Aidha, amekumbusha umuhimu wa kuondoa vikwazo vinavyowakabili wanawake katika sayansi, ikiwa ni pamoja na upungufu wa miundombinu, ukosefu wa vifaa vya kisasa na changamoto za kifedha ambapo alisema kuwa mazingira rafiki na wezeshi yajengwe ili kuwezesha wanawake na wasichana kujifunza bila vikwanzo.
Ametaja baadhi ya maeneo na juhudi mbalimbali zinazofanyika kuongeza ushiriki wa kundi Hilo kuwa ni pamoja na utekelezaji wa Sera mpya ya Elimu na Mafunzo ya 2014 Toleo la 2023 sambamba na mitaala iliyoboreshwa ambapo Serikali imeanza msukumo mkubwa katika kuandaa walimu Bora ,kuwekeza katika mazingira mazuri ya kujifunza na kufundishia likiwemo kundi la wanawake na wasichana.
Hata hivyo amewataka watendaji wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia iangalie ushindani uliopo na utekelezaji wa Sera mpya ya Elimu ya 2014 Toleo la 2023,ijikite katika kutatua changamoto zilizopo katika jamii.
Vile vile Kikwete ametaka ushirikiano wa Sekta ya Umma na sekta binafsi katika kubuni njia na mikakati ya kuimarisha na kuratibu ufungamishaji wa mipango na programu zinazolenga kuongeza ushiriki wa wanawake na wasichana katika STEM na ngazi nyingine za kisayansi.
“Amezitaka sekta hizo kufanya tafiti mahsusi zinazolenga kubainisha hali halisi ya idadi ya wanawake na wasichana wanaojiunga na STEM katika ngazi mbalimbali nchini katika kipindi kisichozidi miaka kumi.”amesema
Katika hatua nyingine amezitaka sekta Binafsi na sekta ya umma kuendesha programu kabambe baina ya sekta ya umma na sekta Binafsi zinazolenga kuleta Mapinduzi katika ushiriki wa michango ya wanawake na wasichana na kuanzisha Mifumo rafiki ya kuvutisha wanawake na wasichana kufanya vizuri katika STEM utafiti na ubunifu nchini.
Aidha  Mhe.Ridhiwani Kikwete amewataka watendaji wa Wizara ya Elimu kuliangalia eneo la Ushindani uliopo na utekelezaji wa Sera mpya ya Elimu ujikite katika kutatua changamoto zilizopo nchini.
Amesema kuwa Serikali inaendelea kutambua changamoto ya Usonji katika jamii yetu, na katika kufanya hilo kupitia Sera Mpya ya Elimu, vijana wenye changamoto ya Usonji ambao ndani yao wana kipaji maalum nalo pia limeangaliwa.
.
“Tunacho chuo cha Patandi ambacho chuo hicho kinaendelea kuwaangalia na kuwafundisha walimu na kukuza vipaji Vya Vijana wenye Usonji, hivyo jambo hilo halijaachwa nyuma” amesema.

       

About the author

mzalendoeditor