Featured Kitaifa

UBORESHAJI WA MITAALA WAWAKOSHA WATANZANIA

Written by mzalendo

Na Mwandishi Wetu, Dodoma. 

BAADHI ya wazazi na walezi katika Wilaya ya Dodoma mjini Mkoani Dodoma wamefurahishwa uanzishwazi wa sera mpya ya elimu ya mwaka 2024 loleo la kwaka 2014 kwa maelezo kuwa ni mkombozi kwa vikana wa Kitanzania.

Wazazi na walezi wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi wamesema kuwa uzinduzi wa sera hiyo inayolenga kuwapatia ujuzi itapunguza changamoto sugu ya ajira.

Fatuma Madida mmoja wa watoto 4 wanaoendelea na masomo kwa hatua mbalimbali amesema serikali imeona kilio cha wazazi wengo kwa kuzindua mtaala mpya ulioboreshwa kwa lengo la kuwasaidia vijana wa kitanzania kwa kuwapatia mafunzo ya ujuzi.

“Nipende kuchukua nafasi kumshukurua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani kwa kuona umuhimu wa kuzindua mtaala mpya kwa wanafunzi wa kitanzania.

“Kama kweli sera hiyo itasimamiwa vizuri sina shaka kuwa vijana wetu watakuwa nanujuzi mkubwa nanuzoefu wa kufanya kazi zao kwa kujiamini tofauti na sasa ambapo vijana wengo wanakosa kazi kwa kigezo cha kukosa uzoefu.

“Tumeona vijana wetu wengi wakishindwa kufanya kazi kwa kigezo kukosa uzoefu,na vijana wamekuwa wanatumia muda mwingi kufanya mafunzo kwa nadharia na muda mfupi utumia kwa vitenda jambo ambalo kwa sasa litaenda kufutika”ameeleza Fatuma.

Kwa upande wake Titto Mwamalala ambaye pia naye ni mzazi amesema kuwa kitendo cha Serikali kuboresha mtaala wa Elimu ni kurejesha heshima ya elimu yenye ujuzi wa taaluma mbalimbali na kuingia katika ushindani wa ajira kimataifa na kitaifa.

MWALIMU MKUU.

Naye mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya New Precious Joseph Shinyanga,amesemankuwa kutokana na uboreshwaji wa mitaala shule hiyo pia itahakikisha inafanya vzuri kwani upatikanaji wa nyenzo kwa maana ya vitabu ni rahisi.

Hata hivyo amesema kuwa anajivunia hatua ya serikali kutoa elimu mbalimbali kwa walimu kwa lengo la kutambua na kupata uelewa sahihi wa utumiaji wa mitaala mipya ya elimu.

Katika kufanikisha ubora wa Elimu Mwalimu Shinyanga amewaomba wazazi na walezi pamoja na walimu kushirikiana kwa ukaribu zaidi wanafunzi ili kuhakikisha uborawa shule hiyo unaboeshwa.

MKURUGENZI.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shule awali na msingi ya New Precious ,Justina William akizungumza na waandishi wa habari ameeleza kuwa kwa sasa elimu ya Tanzania inaenda kuingia katika la ushindani ndani na nje ya Tanzania kwa kuwa na vijana wengi wenye taaluma na uzoefu.

Mkurugenzi huyo ambaye ameeleza kuwa shule yake iliyopo Michese Jijini Dodoma kuwa inapokea wanafunzi wa aina mbalimbali ikiwepo watoto wenye mahitaji maalumu na miundombinu ya mahitaji yao yameboreshwa.

“Shule yangu inapokea watoto wenye mahitaji Mbalimbali na kila mtoto analindwa kulingana na mahitaji yake hivyo wazazi na walezi wenye watoto wenye mahitaji wapelekwe katika shule hiyo.

“Lakini pamoja na mambo mengine bado kuna changamoto mbalimbali kama vile miundombinu ya barabara hivyo tunamuomba Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuona uwezekano wa kusaidia kujenga barabara hata ya changalawe”ameeleza.

Akizungumzia uwekezaji wa watanzania katika Jiji la Dodoma amesema kuwa ni matunda ya Dodoma kutangazwa raam kuwa makao makuu ya nchi.

About the author

mzalendo