Na Mwandishi Wetu Korogwe, Tanga.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) ameshiriki mazishi ya Ndg. Charles Davidi Gawile aliyefariki tarehe 06 Febuari, 2025 naa kuzikwa Wilayani Korogwe Mjini, leo tarehe 09 Febuari, 2025.
Akizungumza na waombolezaji walioshiriki ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la Anglikana *Chatanda,* amesema marehemu *Gawile* atakumbukwa kwa mema na mazuri aliyoyatenda enzi za uhai wake kwa wananchi na Wilaya ya Korogwe na Mkoa wa Tanga kwa ujumla kwa kuwa alikuwa mtu wa watu.