Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi -PPP, Bw. Bashiru Taratibu akitoa ufafanuzi mara baada ya Wasilisho la Utekelezaji wa mkakati wa Sera ya Taifa ya PPP 2021/22-2025/26 (halionekani pichani) kwa wajumbe walioshiriki kikao kazi cha kupitia Marekebisho ya sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi (PPP), pamoja na kupitia utekelezaji wa Mkakati wa Sera ya Taifa ya PPP ya miaka mitano kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam.
Mchumi Mkuu kutoka Wizara ya Fedha, Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi -PPP, Bw. Alfred Misana akitoa ufafanuzi mara baada ya Wasilisho kuhusu dhana ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi -PPP (halionekani pichani) kwa wajumbe walioshiriki kikao kazi cha kupitia Marekebisho ya sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi (PPP), pamoja na kupitia utekelezaji wa Mkakati wa Sera ya Taifa ya PPP wa Miaka Mitano, kilichofanyikakatika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam.
Mchumi kutoka Wizara ya Fedha, Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi – PPP, CPA Fredrick Sanga, akiwasilisha mada (haionekani pichani) kuhusiana na Utekelezaji wa Mkakati wa Sera ya Taifa ya PPP 2021/22-2025/26 iliyoongelea utekelezaji wa Sera ya PPP ya mwaka 2019 pamoja na Mkakati wa kutekeleza Sera ya PPP ya mwaka 2019, katika kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao kazi cha kupitia Marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), pamoja na kupitia Utekelezaji wa Mkakati wa Sera ya Taifa ya PPP wa Miaka Mitano, wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa katika Ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam.
Mchumi Mwandamizi kutoka Tume ya Taifa ya Mipango Bw. Khalid Twaha Shekimweri, akiwasilisha Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma na Waraka Na. 5 wa Hazina wa mwaka 2021/22 (hauonekani pichani), katika kikao kazi cha kupitia Marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi (PPP), pamoja na kupitia utekelezaji wa Mkakati wa Sera ya Taifa ya PPP wa miaka mitano kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam.
Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha, Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Bi. Josephina Buhili (kushoto) akijadiliana jambo na Afisa Sheria Mwandamizi kutoka Kituo cha Ubia Baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi – PPP Centre Bi. Paulina Fungameza, katika kikao kazi cha kupitia Marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi (PPP), pamoja na kupitia Utekelezaji wa Mkakati wa Sera ya Taifa ya PPP wa Miaka Mitano kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)
Na. Eva Ngowi -WF -Dar es Salaam
Wizara ya Fedha kupitia Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi – PPP, imeziasa Wizara na Taasisi zilizoshiriki kikao kazi cha kupitia marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi (PPP), pamoja na kupitia utekelezaji wa Mkakati wa Sera ya Taifa ya PPP ya miaka mitano (2021/22 – 2025/26), kuwa wabunifu wakati wa kuandaa miradi ya PPP.
Hayo yameelezwa na Kaimu Kamishna wa Kitengo cha PPP, Wizara ya Fedha, Bw. Bashiru Taratibu wakati akitoa wasilisho kwa Wizara na Taasisi kuhusiana na Utekelezaji wa Mkakati wa Sera ya Taifa ya PPP ya Miaka Mitano, katika kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Dar es Salam.
Bw. Taratibu alisema kuwa ubunifu ukitumika katika utekelezaji wa majukumu waliyonayo utasaidia kupata vyanzo mbadala vya rasilimali fedha na kupunguza muda wa kusubiri fedha kutoka Serikalini kwa ajili ya kutekeleza miradi maendeleo.
“Kila Taasisi imepewa majukumu mahsusi, yanayotakiwa kufanywa kwa kutumia “resource” (rasilimali)zinazotoka Serikalini, unaweza ukajikuta rating yako kila mwaka inakuwa kwenye kiwango cha chini kwa kuwa unakuwa hupati rasilimali fedha za kutosha na kwa wakati. Kwa hiyo tuwe wabunifu ili kuhakikisha tunapeleka huduma nzuri kwa jamii.” Alifafanua Bw. Taratibu.
Aidha, kikao kazi hicho kilijadili mada mbalimbali zikiwemo; Dhana ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi -PPP, Utekelezaji wa Mkakati wa Sera ya Taifa ya PPP (2021/22-2025/26), Marekebisho ya Sheria ya PPP, Sura 103 na Kanuni za PPP 2023, Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma, Waraka Na.5 na 7 wa Hazina wa Mwaka 2021.
Kikao kazi hicho cha siku sita, kimeshirikisha baadhi ya Wizara na Taasisi zikiwemo Wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Wizara ya Fedha, Wizara ya Afya, Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Uchukuzi na Tume ya Taifa ya Mipango. Taasisi zilizoshiriki ni Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka- DART, Shirika la Maendeleo na Uchumi la Jiji la Dar es Salaam- DDC, Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili – MOI, Taasisi ya Saratani Ocean Road, Wakala wa Barabara Tanzania – TANROADS, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania – TAA, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania – GBT, Wakala wa Majengo Tanzania – TBA na Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA.