Featured Kitaifa

UVCCM CHEMBA WAMPA TANO MBUNGE WAO

Written by mzalendoeditor

Umoja wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM) Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma umempongeza Mbunge wa Jimbo hilo Mohammed Monni kwa kutekeleza na kusimamia ipasavyo miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Wilaya hiyo Ikiwemo Kufungua shule 13 mpya za Msingi, shule 7 mpya za sekondari, Zahanati 11, pamoja na vituo vya afya.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Umoja huo Mhandisi Jalali Mkunji wakati wakikao cha mwisho wa mwaka cha Bazara hilo kilichofanyika Wilayani hapo.

Mhandisi Mkunji amesema Mbunge Monni amefanyakazi kubwa pamoja na kutoa ushirikiano mkubwa kwa chama chetu pamoja na kuisaidia jumuiya yetu kutimiza wajibu wake.

Amesema jitahidi hizi zimefanikiwa kwa sababu Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ametoa fedha jingi na kuzielekeza maeneo yote ya Nchi yetu.

About the author

mzalendoeditor