Featured Kitaifa

TAKUKURU DODOMA YATAJA VIPAUMBELE VYAKE IKIWEMO KUPITIA RIPOTI YA CAG

Written by mzalendoeditor
MKUU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma Bw.Victor Swella,akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 29,2025 jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi ya Taasisi hiyo kwa kipindi cha Oktoba- Disemba 2024.
Na Alex Sonna,Dodoma
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma imetaja vipaumbele vyake katika kipindi cha miezi 3 (Januari- Marchi) ikiwemo kufanya uchunguzi wa tuhuma zilizobainishwa katika  taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
Hayo ameelezwa  leo Januari 29,2025 Jijini Dodoma  na Mkuu wa TAKUKURU  Mkoa wa Dodoma,Victor Swella wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi ya Taasisi hiyo kwa kipindi cha Oktoba- Disemba 2024 kwa Waandishi wa Habari.
Bw.Swella amesema pamoja na utekelezaji wa majukumu mengine pia wamejiwekea malengo ya kutekeleza vipaumbele vinavyolenga kuzuia vitendo vya rushwa visitokee kwa kufanya  uchunguzi za tuhuma zilizobainishwa katika  taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
“Malalamiko ya matumizi mabaya ya Ofisi na mamlaka katika idara ya ardhi katika Jiji la Dodoma na tuhuma zingine kadri zitakavyobainika,”amesema Mkuu huyo wa Takukuru.
Amesema pia wamejipanga kuongeza Kasi ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuziba  mianya ya rushwa na ufujahi unaoweza kujitokeza katika utekelezaji wa miradi.
Mkuu huyo wa Takukuru amesema pia wamejipanga kuongeza Kasi ya uelimishaji Umma kuhusu madhara ya rushwa katika uchaguzi kwa makundi tofauti tofauti katika uchaguzi wa madiwani,wabunge na Rais unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
“Kutoa elimu kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa/ Vijiji na Wajumbe wa Halmashauri za Serikali za Mitaa juu ya wajibu wao katika mapambano dhidi ya rushwa

About the author

mzalendoeditor