Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali inaendelea kutathmini na kukarabati miundombinu ya Barabara zunazosimamiwa na TARURA zilizoathiriwa na mvua za El Nini katika maeneo mbalimbiali nchini ambapo mpaka sasa zaidi ya Bilioni 84 kukarabati baadhi ya maeneo nchini.
Mhe. Katimba amesema hayo bungeni jijini Dododma wakati akijibu swali la Mhe. Francis Kumba Ndulane mbunge wa jimbo la Kilwa Kaskazini aliyetaka kujua ni lini serikali itapelekeka pesa kwaajili ya ukarabati wa madaraja zaidi ya 10 yaliyoathiriwa na mvua hizo katika Barabara ya Mt. Kimwaga Kwenda Kandawale.
Akijibu swali hilo Mhe. Katimba amesema “Serikali inaendelea kufanya mapitio na tathmini ili iweze kufikia maeneo mengi zaidi ambayo yameathirika na mvua za ElNino na madaraja uliyoyataja yatafanyiwa ukarabatina wananchi waweze kupata miundombinu bora” Amesema