Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI

Written by mzalendoeditor

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya  uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu  Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka walioteuliwa ni kama ifuatavyo: 

(i) Mhandisi Ramadhani Masoud Lwamo ameteuliwa kuwa Katibu  Mtendaji wa Tume ya Madini. Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi  Lwamo alikuwa akikaimu nafasi hiyo; 

(ii) Dkt. Aggrey Kalimwage Mlimuka ameteuliwa kuwa Mwenyekiti  wa Bodi ya Tume ya Ushindani (FCC) kwa kipindi cha pili; 

(iii) Prof. Othman Chande Othman ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa  Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kipindi cha pili; 

(iv) Dkt. Florens Martin Turuka ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi  ya Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kwa kipindi cha pili; na 

(v) Prof. Valerian Cosmas Silayo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa  Bodi ya Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini  (CAMARTEC) kwa kipindi cha pili. 

About the author

mzalendoeditor