Featured Kitaifa

MAWAZIRI WATATU WAKUTANA DODOMA KUJADILI SUALA LA UTOAJI WA AJIRA MPYA

Written by mzalendo

Mawaziri watatu wamekutana Jijini Dodoma kujadili suala zima la utoaji wa ajira mpya za Kada ya Ualimu kwa kuzingatia mahitaji ya Sera ya nchi pamoja na Sheria, Kanuni na Taratibu katika zoezi zima la ajira hizo.

Waheshimiwa Mawaziri waliokutana ni Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (Mb) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Mhe. Prof. Adolf Faustine Mkenda Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Kikao cha Mawaziri hao kimefanyika kwenye ukumbi wa Video Conference ulioko kwenye Jengo la Ofisi ya Rais – TAMISEMI leo tarehe 15.01.2025.

About the author

mzalendo