📍30 Disemba, 2024 | IRINGA MJINI
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Taifa, *Ndg. Mary Chatanda (MCC)* amekabidhi Gari jipya lenye thamani ya Milioni 29, likiwa likejazwa Mafuta pamoja na Bima ya Miezi 6 kwa Katibu wa UWT Mkoa wa Iringa Kwa Matumizi ya Ofisi ambalo limenunuliwa na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UWT anayewakilisha Wanawake wa Mkoa wa Iringa *Ndg. Fatma Rembo*.
*Aidha* , Chatanda amempongeza sana Ndg. Fatma Rembo Kwa kazi Kubwa anayoifanya Kwa namna anavyotimiza Majukumu yake kwani UWT Mkoa wa Iringa ilikuwa ikikabiliwa na changamoto ya Usafiri hivyo litakwenda kusaidia katika shughuli za UWT katika kuimarisha Jumuiya.
Mwenyekiti wa UWT Taifa aliyasema hayo Wakati akihitimisha Ziara yake tarehe 30 Disemba, 2024 ziara yake ya siku nne mkoani Iringa. Ziara hiyo ilianza Novemba 27 ikiwa na lengo la kuhamasisha wananchi wa mkoa huo, kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha tarifa zao kwenye daftari la kudumu la mpiga kura.
#uwtimara
#jeshiladktsamianadktmwinyi
#kaziiendelee