Featured Kitaifa

CHATANDA AHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

Written by mzalendo

NA MWANDISHI WETU, IRINGA.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT). *Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC)* amewasisitiza na kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga lilianza leo 27 Disemba, 2024 hadi 02 Januari, 2025 ili waweze kutimiza haki yao ya kuchagua viongozi bora na watakaoleta maendeleo kwa watanzania.

Katika kuelekea uchaguzi Mkuu 2025 Chatanda, amewataka wananchi mkoani Iringa, Mbeya na Wilaya ya Mpwapwa (M) Dodoma kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la mpiga kura ili waweze kuwapata Viongozi Bora watakaowaletea Maendeleo.

Akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Migori Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani humo na kusisitiza kuwa ni muhimu kwa Kila mwananchi mwenye sifa za kushiriki uchaguzi huo ili aweze kuchagua kiongozi ambae anaona ana uwezo wa kuleta Matokeo chanya katika jamii.

“Wito wangu Kwenu wananchi kwenda kuboresha Taarifa zenu katika daftari la mpiga kura kwasababu wasipoenda watakosa haki yao ya msingi ya kupiga kura” Alisema.

*Aidha* alisema Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kuleta mabadiliko makubwa katika jamii kwa kuwaletea Maendeleo wananchi kwa kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa Mkoa wa Iringa na Taifa kwa ujumla, hivyo ili kuunga mkono jitihada hizi zinazofanywa na Serikali chini ya uongozi wake Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, tumemaliza zoezi la uchaguzi wa Serikali za mitaa, hivi sasa tumeingia kwenye kujiandikisha kwenye Daftari la mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi m
Mkuu unaotarajia kufanyika nchini 2025;

Kwa yule ambae hakujiandikisha 2019/20 na ambae umri wake miaka 18 anatakiwa aende akajiandikishe wakiwemo wale wote wenye umri wa miaka 17 ambao mwakani watatimiza miaka 18 nao wanatakiwa wakajiandikishe.

Katika hatua nyingine, aliupongeza uongozi wa CCM Mkoa wa Iringa kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuhamasisha WANANCHI kujiandikisha kwa wingi kwenye daftari la mpiga kura katika Serikali za mitaa na kupelekea mkoa wa Iringa kushika nafasi ya kwanza kitaifa.

“Mkoa wa Iringa umefanya vizuri Sana katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kutokana na hamasa kubwa mliyoitoa kwa wananchi, hakikisheni mnafanya kazi nzuri zaidi inafanyika kuhamasisha wananchi kwenda kujiandikisha ili waweze kuwachagua Viongozi wanaotokana na ccm.

About the author

mzalendo