Featured Kitaifa

SERIKALI KUENDELEA KUDHIBITI WANAOTOA MIKOPO KAUSHA DAMU

Written by mzalendoeditor
Waziri wa Fedha, Mhe, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizingumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Kwanza la Wadau wa Sekta ya Fedha kwa mwaka 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, ambazo ni Mkakati wa Upatikanaji wa Fedha kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Mwaka 2023/24 – 2028/29, Mwongozo wa Mitaji Halaiki (Crowd financing) pamoja na Mwongozo wa Utoaji Hati Fungani zinazozingatia Sharia kwa Kampuni na Taasisi za Umma wa Mwaka 2023 (Capital Markets and Securities (Corporate and Subnational SUKUK Bonds) Guidelines-2023, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Kwanza la Wadau wa Sekta ya Fedha kwa mwaka 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam..
Na Farida Ramadhani na Chedaiwe Msuya, WF – Dar es Salaam.
 
Serikali imesema itaendelea kuchukua hatua kali kwa taasisi zote zininazotoa huduma za fedha kinyume cha sheria kwa kutoa mikopo umiza (kausha damu) na kuwakandamiza wananchi.
 
Onyo hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), wakati akizindua Jukwaa la kwanza la Wadau wa Sekta ya Fedha kwa mwaka 2024. 
 
Dkt. Nchemba alisema taasisi hizo zimekuwa zikiwaumiza wananchi kwa kutoa mikopo yenye riba kubwa pamoja na kupanga njama za kuwafilisi wale ambao wanajua wazi hawatoweza kulipa mikopo hiyo.
 
Aliwataka wadau wa Sekta ya Fedha hususan benki kuendelea kutoa elimu ya umuhimu wa kutumia huduma rasmi za fedha kwa kutumia taasisi ambazo zimesajiliwa ili kuepukana na madhara wanayokumbana nayo katika taasisi nyonyaji zinazotoa mikopo umiza (kausha damu).
 
“Lazima wananchi wajue kutoafautisha kati ya Taasisi rasmi na hizo zisizo rasmi, lazima tuwaoneshe wananchi kuwa hawako salama wanapokopa kwenye taasisi zisizo rasmi na kuwahamasisha kuwa benki ni salama zaidi”, alibainisha Dkt. Nchemba.
 
Alisema ni vema wadau wa Sekta ya Fedha wawaelimishe wananchi kuhusu umuhimu wa kutumia benki kupata mikopo pamoja na kutunza fedha zao kwa kuwa kutunza fedha benki ni utaratibu wa kisasa wa uendeshaji wa uchumi.
 
” Bado kuna baadhi ya maeneo wananchi wanaogopa kuweka fedha benki, kwa kuwa nyinyi mpo kwenye Sekta hii mshirikiane na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwaeleza wananchi kuwa wasiogope kuweka fedha benki ”, alifafanua Dkt. Nchemba.
 
Alisema pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kukusanya kodi kwa weledi na kwa kufuata sheria bado wananchi hawajaeleweshwa vizuri kuhusu kuweka fedha benki.
 
Aliwaagiza viongozi wa Taasisi za Fedha nchini kujiridhisha kabla ya kuruhusu watumishi na madalali wao kupiga minada ya mali za wadaiwa mikopo kwenye Taasisi zao kwa kuwa kuna taarifa kuwa baadhi ya watumishi wasio waaminifu hushirikiana na watu wengine kuwadhulumu mali zilizowekwa kwama dhamana na kuwatia watu umasikini.
 
”Kuna baadhi ya maeneo hakufanyiki vizuri katika kudai mikopo, mteja amelipa mkopo wake kwa asilimia 80, amebakiza asilimia 20, anatokea mteja mwingine anapenda dhamana ya mkopo iliyowekwa, benki inaamua kupiga mnada wa muda mfupi ambao wanajua mteja hatoweza kulipa ili wamfilisi, mtu amelipa mkopo kwa asilimia 80 halafu unauza dhamana yake ili kufidia asilimia 20 ambayo hajalipia huko ni kumtia umaskini, huu sio utaratibu mzuri wa kujenga sekta ya fedha na sio utaratibu mzuri wa kujenga ustawi wa jamii”, aliongeza Dkt. Nchemba.
 
Dkt. Nchemba aliziagiza Benki kuwachukulia hatua kali baadhi ya watumishi wa benki wasio waaminifu ambao wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya wateja kuongeza mikopo chechefu.
 
Aidha, aliwaagiza wadua wa Sekta ya Fedha kuendelea kuwasisitiza wananchi kuwa fedha za mkopo zitumike kwenye shughuli za uzalishaji kwa sababu shughuli zinazoweza kuzalisha ndio zinazoweza kurejesha mkopo huku akitolea mfano nchi inapokopa fedha zinapelekwa kwenye miradi mahusi ya maendeleo,  kwasababu miradi ya maendeleo ndio inaweza kuzalisha na kulipa deni  na haijawahi kukopa kwa ajili ya kulipa mishahara.
 
Alisema kutokana na kupeleka fedha kwenye miradi ya maendeleo ndio maana Tanzania ni miongoni mwa nchi mbili pekee barani Afrika zenye uhimilivu wa deni na kwa Afrika Mashariki na nchi zilizopo katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), 
Tanzania inaongooza.
 
Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda alisema mwakani Serikali itaanzisha Mtaala Mpya wa masomo ambapo somo la masuala ya fedha na ujasiriamali litakuwa ni la lazima ili kuwaezesha wanafunzi watakapo maliza masomo yao kuweza kujiajiri.
 
Aliwataka wadau mbalimbali kuendelea kutoa maoni kuhusu mtaala huo ili kuuwezesha kufikia lengo kusudiwa.
 
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba alisema Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau wa Sekta ya Fedha nchini imeandaa Jukwaa la wadau wa Sekta ya Fedha ili kubadilishana mawazo na uzoefu, kupeana taarifa, kujengeana uwezo, kushirikishana katika mafanikio na changamoto na kutafuta suluhu ya pamoja kwa changamoto zinazoikabili sekta ya fedha nchini.
 
Alisema malengo ya Jukwaa la Wadau wa Sekta ya Fedha kwa mwaka 2024 ni pamoja na kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kipindi cha miaka mitatu (2020/21-2023/24) na kushirikishana mbinu bora za kiutendaji na uzoefu katika Sekta ya Fedha.
 
Dkt. Mwamba alisema malengo mengine ni kujadili fursa na hatua mbalimbali zilizochukuliwa katika kuboresha sekta ya Fedha pamoja na kushirikishana namna bora ya kukuza matumizi ya teknolojia na uvumbuzi ili kukuza na kuimarisha Sekta ya Fedha.
Aliongeza kuwa Jukwaa hilo pia linalenga kuimarisha ushirikiano miongoni mwa wadau wa Sekta ya Fedha na kuufahamisha Umma juu ya hatua za maboresho mbalimbali ya kisera na kisheria yaliyofanyika ili kuimarisha Sekta ya Fedha nchini.
Waziri wa Fedha, Mhe, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Katikati), akizindua moja ya nyaraka zilizoandaliwa za Sekta ya Fedha ambazo ni Mkakati wa Upatikanaji wa Fedha kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Mwaka 2023/24 – 2028/29, Mwongozo wa Mitaji Halaiki (Crowd financing) pamoja na Mwongozo wa Utoaji Hati Fungani zinazozingatia Sharia kwa Kampuni na Taasisi za Umma wa Mwaka 2023 (Capital Markets and Securities (Corporate and Subnational SUKUK Bonds) Guidelines-2023, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Kwanza la Wadau wa Sekta ya Fedha kwa mwaka 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizingumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Kwanza la Wadau wa Sekta ya Fedha kwa mwaka 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, ambazo ni Mkakati wa Upatikanaji wa Fedha kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Mwaka 2023/24 – 2028/29, Mwongozo wa Mitaji Halaiki (Crowd financing) pamoja na Mwongozo wa Utoaji Hati Fungani zinazozingatia Sharia kwa Kampuni na Taasisi za Umma wa Mwaka 2023 (Capital Markets and Securities (Corporate and Subnational SUKUK Bonds) Guidelines-2023, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Kwanza la Wadau wa Sekta ya Fedha kwa mwaka 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam..
Waziri wa Fedha, Mhe, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (wa tatu kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (watatu kulia), Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Sauda Msemo (wapili kushoto) wakiwa pamoja na viongozi wengine wa Serikali, wakionesha nyaraka zilizoandaliwa za Sekta ya Fedha ambazo ni Mkakati wa Upatikanaji wa Fedha kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Mwaka 2023/24 – 2028/29, Mwongozo wa Mitaji Halaiki (Crowd financing) pamoja na Mwongozo wa Utoaji Hati Fungani zinazozingatia Sharia kwa Kampuni na Taasisi za Umma wa Mwaka 2023 (Capital Markets and Securities (Corporate and Subnational SUKUK Bonds) Guidelines-2023, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Kwanza la Wadau wa Sekta ya Fedha kwa mwaka 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam

   

Wadau mbalimbali wa Sekta ya Fedha, wakifuatilia hotuba ya Ufunguzi ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), wakati akizundua Jukwaa la Kwanza la Wadau wa Sekta ya Fedha kwa mwaka 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, ambapo alitumia fursa hiyo ambazo ni Mkakati wa Upatikanaji wa Fedha kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Mwaka 2023/24 – 2028/29, Mwongozo wa Mitaji Halaiki (Crowd financing) pamoja na Mwongozo wa Utoaji Hati Fungani zinazozingatia Sharia kwa Kampuni na Taasisi za Umma wa Mwaka 2023 (Capital Markets and Securities (Corporate and Subnational SUKUK Bonds) Guidelines-2023, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Kwanza la Wadau wa Sekta ya Fedha kwa mwaka 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Kwanza la Wadau wa Sekta ya Fedha kwa mwaka 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, ambapo aliipongeza Wizara ya Fedha kwa kuandaa Jukwaa hilo na kwamba Wizara yake imetambua umuhimu wa masuala ya uchumi na fedha na imeandaa Mtaala Mpya wa Elimu utakao wawezesha wanafunzi kupata elimu ya ujasiriamali pamoja na biashara ili kuwajengea maarifa ya kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Kwanza la Wadau wa Sekta ya Fedha kwa mwaka 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau wa Sekta ya Fedha nchini imeandaa Jukwaa hilo ili kubadilishana mawazo na uzoefu, kupeana taarifa, kujengeana uwezo, kushirikishana katika mafanikio na changamoto na kutafuta suluhu ya pamoja kwa changamoto zinazoikabili sekta ya fedha nchini.
 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)

About the author

mzalendoeditor