Wafanyakazi wa Barrick wakishangilia mafanikio ya kampuni baada ya ushindi wa Tuzo za ATE katika vipengele mbalimbali
Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Apolinary Lyambiko (kushoto) akipokea kikombe cha Tuzo ya Ushindi wa Mwajiri bora ilipopokelewa mgodini.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Apolinary Lyambiko (kushoto) akipokea kikombe cha Tuzo ya Ushindi wa Mwajiri bora ilipopokelewa mgodini.
**
Mgodi wa North Mara unaoongoza kuwa taswira ya mafanikio mbalimbali katika uwekezaji wa sekta ya madini upo wilayani Tarime mkoani Mara na umeanza kufanya uzalishaji chini ya kampuni ya Barrick yenye ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals mnamo mwaka 2019.
Moja ya mafanikio ambao mgodi huo umepata karibuni kati ya mafanikio yake mengi ni kuibuka mshindi katika tuzo kubwa ya jumla katika Tuzo za Mwajiri Bora 2024 ambazo zinatolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ukiwa ni mwendelezo wa rekodi ya ushindi huo mwaka jana pia uliibuka kidedea katika tuzo hizo.
Mbali na ushindi wa jumla North Mara katika tuzo hizi mwaka huu pia imeweza kushinda tuzo katika vipengele vya uwajibikaji kwa jamii (CSR),utekelezaji sera ya maudhui ya ndani kwa ufasaha-Local content, Afya na Usalama Mahali pa kazi, Mwajiri Bora katika sekta binafsi.
Ni dhahiri kuwa mafanikio makubwa ambayo North Mara inaendelea kuyapata yanatokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni ya Barrick inayoendesha mgodi huo kwa ubia na Serikali ya Tanzania sambamba kuwa na timu ya wafanyakazi wenye utaalamu na weredi mkubwa ambao pia wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.
Tuzo ya Jumla ya Mwajiri bora
Tuzo hii kubwa imetokana na mgodi huu ambao unaendesha shughuli zake kwa viwango vya kimataifa kuweza kuzalisha ajira nyingi za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja nchini na maeneo yanayozunguka mgodi, ndio maana pia umepata tuzo ya Mwajiri bora katika sekta binafsi.
Mgodi umeweza kuchochea fursa za ukuaji wa uchumi kupitia kodi mbalimbali na tozo unaolipa Serikalini.Mwaka juzi uliweza kuibuka kinara wa kulipa kodi nchini na kutunukiwa tuzo ya Mlipa kodi bora na Mamlaka ya Mapato nchini na umekuwa ukiendelea kuchangia uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa.
Uwajibikaji kwa Jamii (CSR)
Mgodi huu kila mwaka umekuwa ukitoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya kufanikisha miradi mbalimbali kupitia fedha za Uwajibikaji kwa jamii, Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Mgodi huo Apolinary Lyambiko, wakati akitoa taarifa ya utendaji wa mgodi kwa waandishi wa habari karibuni, alisema Barrick North Mara katika kipindi cha mwaka huu wa 2024 imetoa kiasi cha bilioni 9 kwa ajili ya kutekeleza miradi 101 ya maendeleo kwenye vijiji 11 vinavyozunguka mgodi katika sekta ya afya, elimu,miundombinu ya maji na shughuli nyingine za kijamii.
Alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2022 na 2023 mgodi umewezesha kukamilika kwa miradi 115 ya maendeleo ya kijamii iliyogharimu takribani shilingi bilioni 7.3 .Kati ya mwaka 2020 hadi 2024 mgodi umewekeza kiasi cha shilingi bilioni 22 katika kutekeleza miradi 253 ya kijamii.
Afya na Usalama mahali pa kazi
Suala la afya na usalama mahali pa kazi ni moja ya sera ambayo imekuwa ikipewa kipaumbele kikubwa katika mgodi wa Barrick North Mara na inatekelezwa kwa vitendo kuanzia kwenye sehemu ya kazi mpaka nje ya sehemu ya kazi lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha kila mtu yupo salama wakati wote.
Katika kuhakikisha usalama kwa kila mmoja mgodi wa Barrick North Mara umekuwa ukishiriki katika maonesho ya Afya na Usalama sehemu za kazi yanayofanyika kila mwaka na kutumia fursa hiyo kutoa elimu ya usalama kwa Wananchi.
Migodi ya Barrick imekuwa ikitekeleza sera ya Journey to Zero inayolenga kuhakikisha Wafanyakazi wake wote wanakuwa salama wanapokuwa salama hadi wanaporudi nyumbani ambapo sasa kampeni hii imevuka mpaka na kupelekwa kwenye jamii ndio maana mgodi umekuwa kinara wa kutoa mafunzo ya usalama kwenye jamii na kufanikiwa kushinda tuzo za OSHA kwenye vipengele mbalimbali kikiwemo kipengele cha kuwajali watu wenye mahitaji maalum.
Maudhui ya Ndani-Local content
Mgodi wa North Mara, umekuwa kinara wa kutekeleza sera ya Serikali ya Maudhui ya ndani (Local content) kwa lengo la kunufaisha wazawa ambapo asilimia kubwa ya wazabuni wake ni wazawa ,mbali na zabuni pia inatekelezwa katika suala zima la ajira na kwenye utekelezaji wa miradi ya kijamii kupitia fedha za CSR.
Katika kudhihirisha jambo hili wafanyabiashara wengi katika miji inayozunguka mgodi huu na sehemu nyinginezo nchini wameweza kukua kibiashara na kufanya uwekezaji kutokana na kufanya biashara na mgodi.
Kwa ajili ya kufanikisha suala hili kwa ufasaha zaidi , Mgodi unao programu ya kuendeleza wafanyabiashara wazawa ijulikanayo kama Local Business Development Program (LBDP) ambayo imewafikia wafanyabiashara wengi na kuwanufaisha.
Ushindi katika vipengele vya tuzo hizi muhimu zinazoenda sambamba na ukuzaji wa uchumi wa nchi na jamii unadhihirisha kuwa ni North Mara ni mfano wa uwekezaji madhubuti katika tasnia ya madini nchini.