Featured Kitaifa

PICHA-KAMATI YA FEDHA, UCHUMI NA BIASHARA YAKUTANA KUJADILI MUUNGANO

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akiongoza kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) cha kujadili masuala ya Muungano kilichofanyika jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Hamza Hassan Juma, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Bw. Salhina Mwita Ameir.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) akishiriki kikao cha Kamati ya Pamoja ya Fedha na Uchumi SJMT na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)  kilichofanyika jijini Dodoma. Wengine kuanzia kulia ni Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Hamza Hassan Juma ambaye ni Mwenyekiti mwenza akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) cha kujadili masuala ya Muungano kilichofanyika jijini Dodoma.

Naibu Makatibu Wakuu Ofisi ya Makamu wa Rais wa pili kulia ni Bw. Abdallah Hassan Mitawi (Muungano) na Bi. Christina Mndeme wakifuatilia kikao cha Kamati ya Pamoja ya Fedha na Uchumi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)  kilichofanyika jijini Dodoma. Wengine kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Jenifa Omolo.

Wataalamu kutoka Wizara za Kisekta na Taasisi mbalimbali za wakishiriki kikao cha Kamati ya Pamoja ya Fedha na Uchumi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichofanyika jijini Dodoma

About the author

mzalendoeditor