Featured Kitaifa

MHANDISI MWAJUMA ATAKA WADAU SEKTA YA MAJI KUTOA MAONI DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri, akizungumza wakati akifungua kongamano la wadau wa sekta ya Maji lililoandaliwa na Wizara ya maji kwa ajili ya  kupokea maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri,(hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la wadau wa sekta ya Maji lililoandaliwa na Wizara ya maji kwa ajili ya  kupokea maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Na.Alex Sonna-DODOMA

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri,amewataka wadau wa Sekta ya maji  kutoa maoni yatakayosaidia kuboresha sekta hiyo kwa miaka 25 ijayo

Mhandisi Waziri ameyasema hayo leo Oktoba 10,2024 jijini Dodoma  wakati akifungua kongamano la wadau wa sekta ya Maji lililoandaliwa na Wizara ya maji kwa ajili ya  kupokea maoni kuhusu dira ya taifa ya maendeleo 2050.

Mhnadisi amesema  kuwa azma ya serikali ni kuhakikisha maji safi na salama yanawafikia wananchi wa mijini na vijijini.

“Uandaaji wa dira utashirikisha makundi mbalimbali, wadau wa maendeleo na sekta binafsi, dira kuu ya maendeleo ya mwaka 2025 ilikuwa na nguzo kuu nne ikiwa ni pamoja na kuboresha maisha ya wananchi, kujenga utawala bora wa sheria na Uchumi imara, dira iliweka viashiria vya kupima kila lengo,” amesema

Pia Mhandisi Waziri amesema hadi kufikia Disemba 2023 Takwimu ya idadi ya watu wanaopata maji safi na salama Vijijini ni asilimia 79 huku Mijini ni asilimia 90.

“Mafanikio ya sekta ya maji yanatokana na mchango mkubwa unaotolewa na wadau wa sekta ya maji, wadau wa maendeleo, taasisi za fedha nje na ndani ya nchi.

Amesema kuwa sekta hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uchafuzi wa Mazingira na uvamizi wa vyanzo vya maji, wanapotoa maoni wazingatie changamoto hizo.

“Kutokana na uzoefu na weledi nina Imani mtatoa maoni kwa mustakabali wa sekta hii miaka 25 ijayo,” amesema Mhandisi Waziri

Wadau walioshiriki kongamano hilo wanatoka makundi mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Rais Tamisemi, Wizara ya afya, wizara ya elimu sayansi na teknolojia, Wizara ya Kilimo na wawakilishi kutoka wizara ya nishati

Wawakilishi wa Taasisi zilizo chini ya wizara ya Maji,Mameneja wa RUWASA wa mikoa na Wilaya.

Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji, wakurugenzi wa bodi za maji za mabonde, Chuo cha Maji, Mfuko wa Taifa wa Maji, wawakilishi wa taasisi za umma ikiwemo tume ya taifa ya Mipango, TANAPA, TFS, EWURA, TANESCO

Wadau wa maendeleo, wadau kutoka taasisi za kidini, Asasi za Kiraia, Taasisi zisizo za kiserikali taasisi zinazojumuisha wakandarasi, washauri, na viwanda vya uzalishaji wa maji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya maji Prospar Mkama amesema mipango ya wizara ya maji ni kuhakikisha wanapeleka huduma ya maji maeneo muhimu ya uwekezaji ili kuendelea kuwavutia Wawekezaji

Kazi kubwa pia ni kuhakikisha tunatengeneza mazingira mazuri kwa wawekezaji ili wavutiwe kuwekeza nchini ni lazima miundombinu ya umeme, barabara na maji ziwe vizuri ili kuwarahisishia wawekezaji, “ameeleza Mkama

About the author

mzalendoeditor