Featured Kitaifa

MISHENI YA UANGALIZI WA UCHAGUZI YA SADC NCHINI MSUMBIJI YAZINDULIWA RASMI

Written by mzalendoeditor

Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akizindua rasmi Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi tarehe 03 Oktoba 2024 katika hafla iliyofanyika jijini Maputo. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini Msumbiji unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024

……………

Rais Mstaafu wa
Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume
amezindua rasmi Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi  leo tarehe 03 Oktoba 2024 katika hafla iliyofanyika
jijini Maputo.

Akizungumza wakati
wa uzinduzi huo uliowashirikisha wadau mbalimbali muhimu wakiwemo Mabalozi
wanaowakilisha nchi zao nchini Msumbiji, Wawakilishi kutoka Serikali ya
Msumbiji, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Msumbiji (CNE), Vyama vya Siasa,
Viongozi wa Dini, Jumuiya za Kiraia na waandishi wa habari, Mhe. Dkt. Karume
ameishukuru Serikali ya Msumbiji kwa kuialika Misheni hiyo ambayo ina jukumu la
kuangalia namna misingi ya demokrasia, taratibu na kanuni za uchaguzi za SADC
zinavyotekelezwa.

Amesema Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC pamoja na mambo mengine itatathmini mwenendo wa uchaguzi kulingana na  Kanuni na Miongozo ya SADC inayoongoza Uchaguzi wa Kidemokrasia iliyorekebishwa mwaka 2021 na kuridhiwa na Nchi Wanachama.

Amesema pamoja na mambo
mengine, Kanuni na Miongozo hiyo inazitaka nchi wanachama kushirikisha
wananchi  katika mchakato wa demokrasia,
kuwawezesha  wananchi kufurahia  haki za binadamu na kuwa huru katika
kushirikiana, kukusanyika  na kujieleza. Kadhalika
kanuni na miongozo hiyo imeweka mikakati ya kuzuia rushwa, upendeleo, migogoro
ya kisiasa, kutovumiliana na kuhakikisha zinakuwepo fursa sawa  kwa vyama vyote vya siasa katika kutumia
vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Serikali na kuhakikisha  uhuru wa wananchi kupata taarifa kuhusu
masuala ya uchaguziunazingatiwa.

Mhe. Dkt. Karume pia
alitumia fursa hiyo kupongeza kazi kubwa iliyofanywa  na Misheni ya Ulinzi wa Amani ya SADC nchini
Msumbiji (SAMIM), ambayo ilifanikiwa kudhibiti
vikundi vya kigaidi vilivyoibka katika maeneo ya Kaskazini mwa Msumbiji
na kuishukuru Serikali ya Msumbiji kwa kuahidi kuendelea kulinda mafanikio
yaliyofikiwa na SAMIM katika eneo hilo.

Vilevile, Mhe. Dkt. Karume
alilipongeza Jeshi la Ulinzi la Msumbiji na vyombo vingine vya Usalama vya nchi
hiyo kwa jitihada zao zilizofanikisha Wananchi katika maeneo ya Kaskazini mwa
nchi hiyo wanajiandikisha kwa ajii ya kupiga kura licha  ya changamoto za kiusalama.

Mhe. Dkt. Karume alitumia
nafasi hiyo pia kuwatakia uchaguzi wa amani na utulivu wananchi wa Msumbiji na
kutoa wito kwa wale wote waliojiandikisha kujitokeza  kwa wingi siku ya tarehe 09 Oktoba 2024 na
kupiga kura. Pia alitoa rai kwa wadau wote wa siasa nchini Msumbiji kuheshimu
maoni na mitazamo tofauti ya kisiasa miongoni mwao na kujua wajibu wao katika
kipindi chote cha uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Naye Mkurugenzi wa Asasi
ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Prof. Kula Ishmael Theletsane alieleza umuhimu wa
Misheni za Uangalizi kuwa zinalenga
kufikia malengo  mahsusi ya mafanikio
hususan kwa mtangamano wa SADC kupitia kanuni ya ustahimilivu, utekelezaji wa
demokrasia, utwala bora na amani.

Misheni  ya SADC, iliwasili nchini Msumbiji tarehe 24
Septemba, 2024 na itakuwepo nchini humo hadi tarehe 20 Oktoba, 2024 kwa lengo
la kuangalia uchaguzi kwa mujibu  wa
Kanuni na Miongozo ya SADC inayoongoza Uchaguzi
wa Kidemokrasia iliyorekebishwa mwaka 2021.

Misheni hiyo ya SADC ina
jumala ya wajumbe 97 ambapo miongoni mwao 52 ni waangalizi wa uchaguzi ambao
watasambazwa kwenye majimbo 11 ya uchaguzi nchini Msumbiji ambayo ni Cabo
Delgado, Nampula, Niassa, Maputo City, Maputo, Tete, Gaza, Inhambane, Sofala,
Manica na Zambezia.

Waangalizi hao wanatoka
katika Nchi 10 ambazo ni wanachama wa SADC. Nchi hizo ni Tanzania, Angola,
Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Eswatini, Malawi, Namibia, Afrika
Kusini, Zambia na Zimbabwe.

Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akizindua rasmi Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi tarehe 03 Oktoba 2024 katika hafla iliyofanyika jijini Maputo. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini Msumbiji unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024

Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akizindua rasmi Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi tarehe 03 Oktoba 2024 katika hafla iliyofanyika jijini Maputo. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini Msumbiji unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024
 
Mkurugenzi wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama , Prof. Kula Ishmael Theletsane akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC nchini Msumbiji. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini humo unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024

Mjumbe wa Troika ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa akichangia jambo wakati wa uzinduzi wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC nchini Msumbiji. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini humo unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024
 
Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akizungumza na na Waangalizi 52 wa SADC kwa lengo la kuwaaga kabla ya kusambazwa katika majimbo 11 ya uchaguzi nchini Msumbiji kwa ajili ya kuangalia uchaguzi. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini Msumbiji unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024

Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mhe. Phaustine Kasike akishiriki hala ya uzinduzi wa 

Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC nchini Msumbiji. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini humo unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024
Mjumbe wa Troika ambaye pia ni Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika masuala ya Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Sofia Mjema akishiriki hafla ya uzinduzi wa

Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC nchini Msumbiji. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini humo unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024
Mjumbe wa Troika ambaye ni Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Talha Waziri akifuatilia uzinduzi wa 

Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC nchini Msumbiji. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini humo unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024
Sehemu ya Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa

Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC nchini Msumbiji. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini humo unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024

Sehemu nyingine ya waangalizi
Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC nchini Msumbiji wakishiriki uzinduzi wa 

Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC nchini Msumbiji. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini humo unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024
Sehemu nyingine ya waangalizi wa uchaguzi 
Meza kuu katika picha ya pamoj
Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao Msumbiji walioshiriki hafla ya uzinduzi wa misheni hiyo
Picha ya pamoja ya kundi la waangalizi wa uchaguzi
Picha ya pamoja ya waangalizi wa uchaguzi
 
Wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi

About the author

mzalendoeditor