Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akizindua rasmi Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi tarehe 03 Oktoba 2024 katika hafla iliyofanyika jijini Maputo. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini Msumbiji unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024
……………
Rais Mstaafu wa
Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume
amezindua rasmi Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi leo tarehe 03 Oktoba 2024 katika hafla iliyofanyika
jijini Maputo.
Akizungumza wakati
wa uzinduzi huo uliowashirikisha wadau mbalimbali muhimu wakiwemo Mabalozi
wanaowakilisha nchi zao nchini Msumbiji, Wawakilishi kutoka Serikali ya
Msumbiji, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Msumbiji (CNE), Vyama vya Siasa,
Viongozi wa Dini, Jumuiya za Kiraia na waandishi wa habari, Mhe. Dkt. Karume
ameishukuru Serikali ya Msumbiji kwa kuialika Misheni hiyo ambayo ina jukumu la
kuangalia namna misingi ya demokrasia, taratibu na kanuni za uchaguzi za SADC
zinavyotekelezwa.
Amesema Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC pamoja na mambo mengine itatathmini mwenendo wa uchaguzi kulingana na Kanuni na Miongozo ya SADC inayoongoza Uchaguzi wa Kidemokrasia iliyorekebishwa mwaka 2021 na kuridhiwa na Nchi Wanachama.
Amesema pamoja na mambo
mengine, Kanuni na Miongozo hiyo inazitaka nchi wanachama kushirikisha
wananchi katika mchakato wa demokrasia,
kuwawezesha wananchi kufurahia haki za binadamu na kuwa huru katika
kushirikiana, kukusanyika na kujieleza. Kadhalika
kanuni na miongozo hiyo imeweka mikakati ya kuzuia rushwa, upendeleo, migogoro
ya kisiasa, kutovumiliana na kuhakikisha zinakuwepo fursa sawa kwa vyama vyote vya siasa katika kutumia
vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Serikali na kuhakikisha uhuru wa wananchi kupata taarifa kuhusu
masuala ya uchaguziunazingatiwa.
Mhe. Dkt. Karume pia
alitumia fursa hiyo kupongeza kazi kubwa iliyofanywa na Misheni ya Ulinzi wa Amani ya SADC nchini
Msumbiji (SAMIM), ambayo ilifanikiwa kudhibiti
vikundi vya kigaidi vilivyoibka katika maeneo ya Kaskazini mwa Msumbiji
na kuishukuru Serikali ya Msumbiji kwa kuahidi kuendelea kulinda mafanikio
yaliyofikiwa na SAMIM katika eneo hilo.
Vilevile, Mhe. Dkt. Karume
alilipongeza Jeshi la Ulinzi la Msumbiji na vyombo vingine vya Usalama vya nchi
hiyo kwa jitihada zao zilizofanikisha Wananchi katika maeneo ya Kaskazini mwa
nchi hiyo wanajiandikisha kwa ajii ya kupiga kura licha ya changamoto za kiusalama.
Mhe. Dkt. Karume alitumia
nafasi hiyo pia kuwatakia uchaguzi wa amani na utulivu wananchi wa Msumbiji na
kutoa wito kwa wale wote waliojiandikisha kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 09 Oktoba 2024 na
kupiga kura. Pia alitoa rai kwa wadau wote wa siasa nchini Msumbiji kuheshimu
maoni na mitazamo tofauti ya kisiasa miongoni mwao na kujua wajibu wao katika
kipindi chote cha uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Naye Mkurugenzi wa Asasi
ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Prof. Kula Ishmael Theletsane alieleza umuhimu wa
Misheni za Uangalizi kuwa zinalenga
kufikia malengo mahsusi ya mafanikio
hususan kwa mtangamano wa SADC kupitia kanuni ya ustahimilivu, utekelezaji wa
demokrasia, utwala bora na amani.
Misheni ya SADC, iliwasili nchini Msumbiji tarehe 24
Septemba, 2024 na itakuwepo nchini humo hadi tarehe 20 Oktoba, 2024 kwa lengo
la kuangalia uchaguzi kwa mujibu wa
Kanuni na Miongozo ya SADC inayoongoza Uchaguzi
wa Kidemokrasia iliyorekebishwa mwaka 2021.
Misheni hiyo ya SADC ina
jumala ya wajumbe 97 ambapo miongoni mwao 52 ni waangalizi wa uchaguzi ambao
watasambazwa kwenye majimbo 11 ya uchaguzi nchini Msumbiji ambayo ni Cabo
Delgado, Nampula, Niassa, Maputo City, Maputo, Tete, Gaza, Inhambane, Sofala,
Manica na Zambezia.
Waangalizi hao wanatoka
katika Nchi 10 ambazo ni wanachama wa SADC. Nchi hizo ni Tanzania, Angola,
Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Eswatini, Malawi, Namibia, Afrika
Kusini, Zambia na Zimbabwe.
Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akizindua rasmi Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi tarehe 03 Oktoba 2024 katika hafla iliyofanyika jijini Maputo. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini Msumbiji unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024
|
Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mhe. Phaustine Kasike akishiriki hala ya uzinduzi wa
|
Mjumbe wa Troika ambaye pia ni Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika masuala ya Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Sofia Mjema akishiriki hafla ya uzinduzi wa
|
Mjumbe wa Troika ambaye ni Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Talha Waziri akifuatilia uzinduzi wa
|
Sehemu ya Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa
|
Sehemu nyingine ya waangalizi |
Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC nchini Msumbiji wakishiriki uzinduzi wa
|
Meza kuu katika picha ya pamoj |
Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao Msumbiji walioshiriki hafla ya uzinduzi wa misheni hiyo |
Picha ya pamoja ya kundi la waangalizi wa uchaguzi |
Picha ya pamoja ya waangalizi wa uchaguzi |
Wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi |