Featured Kitaifa

BIL. 6.7 ZABORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU – MUHEZA’ MHE. KATIMBA

Written by mzalendo

Zaidi ya shilingi bilioni 6.7 zimetumika katika ujenzi wa shule za sekondari 10 katika wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga katika kipindi cha maka mitatu ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Shule hizo zimejengwa katika kata 10 kati ya 13 za wilaya hiyo ili kusogeza huduma kwa wakazi wa maeneo hayo ambao watoto wao walikuwa wanatembea umbali mrefu kwaajili ya masomo sababu iliyokuwa inasababisha matokeo mabaya katika mitihani ya Elimu ya sekondari.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba katika uzinduzi wa Kampeni ya Mtoto wa Leo Samia wa Kesho iliyolenga kuibua vipaji vya watoto na kuwatambua watoto wenye ulemavu katika wilaya ya Muheza
mkoa wa Tanga na mgeni rasmi akiwa Mhe. Dkt. Doto Biteko,Naibu Waziri Mkuu na Waziri Nishati.

“Hapo awali kulikuwa na kata 13 ambazo hazikuwa na shule za sekondari lakini alivyoingia madarakani Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshaleta fedha ambazo zimejenga shule za sekondari katika kata 10 na mwaka huu wa bajeti kuna kata
nyingine ya Kwezitu ambayo na yenyewe imeletewa milioni 580 kwaajili ya kujenga shule ya sekondari na tafsiri yake ni zimebaki kata mbili tu” Amesema

Katika Hatua nyingine Mhe. Katimba amempongeza Mbunge wa Jimbo la Muheza Mhe. Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ kwa kushirikian na rafiki zake kwa kujenga shule yenye madarasa sita,vyoo na Ofisi katika kata ya Magoroto ambayo mwaka 2025 itaanza kupokea wanafunzi.

Amesema seikali inaendelea kuimarisha sejkta ya elimu kwa kuendelea kutoa mafunzo kwa walimu na kuwajengea nyumba za kuishi ili wheeze kufanya kazi kwa bidii na ubunufu katika sekta ya elimu.

Akizungumzia mafanikio katika sekta ya Elimu katika Jimbo la Muheza,mbunge wa Jimbo hilo Hamis Mwinjuma amesema ndani ya miaka mitatu jumla ya vyumba vya madarasa 212 na amemshukru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa alama
aliyoiweka katika wilaya ya Muheza.

Akihutubia wananchi wa Muheza waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni ya Mtoto wa Leo Samia wa Kesho Naibu Waziri Mkuu na Waziri na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amehimiza wananchi kuendelea kuilinda miundombinu hiyo huku akiwataka walimu kuwa wabunifu katika ufundishaji ili watoto wapate uelewa na kuwapata Samia wa kesho.

About the author

mzalendo