Featured Kitaifa

“MAHABA MAKUBWA KWA RAIS SAMIA MKOANI RUVUMA” HII NI MAJIMAJI!

Written by mzalendoeditor

NI MAHABA MAKUBWA!
Maelfu ya wananchi kutoka mkoa wa Ruvuma na maeneo yake wametokelezea kwa wingi, wakiwa na hamasa na furaha tele, kumshuhudia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, akihutubia katika mkutano mkubwa uliofanyika Uwanja wa Majimaji mjini Songea tarehe 28 Septemba 2024. Mkutano huu unahitimisha ziara yake ya siku sita mkoani hapa ya kukagua maendeleo na jinsi Ilani ya CCM inavyotekelezwa.        

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwaaga wananchi mara baada ya kumaliza mkutano wa kuhitimisha ziara yake katika uwanja wa Majimaji, Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma tarehe 28 Septemba, 2024.

   

About the author

mzalendoeditor