Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza katika mkutano wa pamoja wa wananchi na watumishi wa Ardhi ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Kilimanjaro
Sehemu ya watumishi wa sekta ya ardhi mkoa wa Kilimanjaro katika kikao chao na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Kilimanjaro
Na MwandishI Wetu
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. Geophrey Pinda amesema kuwa hakuna afisa Ardhi atakayehamishwa eneo la kazi endapo atakiuka maadili ya utendaji wa taaluma yake.
Amesema hayo Septemba 19, 2024 katika mkutano wa pamoja wa wananchi na watumishi wa Ardhi ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Kilimanjaro.
“Nikimwambia Katibu Mkuu huyu utendaji kazi wake unaripotiwa kwamba hafai tutatuma vyombo vitakuja kukutafakari upya”.
“Usikubali kwenye dawati lako kiwe chanzo cha mgogoro upelekwe kwa Mkuu wa Wilaya (DC) kwa Mkurugenzi, kwa Mbunge na jamno lile ulilolianzisha wewe linaenda mpaka kwa Rais! Haiwezekani kila mtu akitafakari”. Amesema mhe Pinda
Aidha, ametoa maelekezo kwa ofisi za Wasajili wa Hati nchini kuharakakisha mchakato wa utoaji hatimiliki za Ardhi ili wananchi waweze kunufaika nazo ikiwa pamoja na kuaminiwa kupata mikopo katika taasisi za kifedha.
“Maelekezo ninayoyatoa kwenye dawati la usajili usilaze kazi toeni hati ziende kwa wananchi “. Amesema mhe. Pinda
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ardhi amewaonya Maafisa Ardhi wanaojiuhusisha l na ugawaji kiwanja kimoja mara mbili na kusisitiza kuwa Wizara yake itachukua hatua kali za kinidhamu dhidi ya mtumishi yeyote atakayekiuka maadili ya utumishi wa umma kwa taaluma yake.
“Kama litamhusisha Afisa wa kwetu kwenye jambo la kugawa kiwanja kimoja mara mbili, sasa hivi hatunamswalia Mtume tutachukua hatua kali” amesema Naibu Waziri Pinda.
Naibu Waziri Mhe. Pinda amehitimisha ziara yake mkoani Kilimanjaro jana ambapo mbali mambo mengine alisikiliza na kutatua changamoto za ardhi kwa wananchi wa mkoa huo pamoja na kufanya vikao kazi na watumishi wa Ardhi mkoani humo.