Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Justine Nyamoga, imeridhishwa na namna ambavyo miradi mbalimbali ya afya na miundombinu ya barabara imetekelezwa katika Halmasahuri ya Wiliya ya Wanging`ombe na kusisitiza kuwa miradi yote lazima iende sambamba na thamani yake ya fedha.
Amesema kumekuwa na miradi mbalimbali ya afya na miundombinu ya Barabara inatekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini lakini kuna baadhi ya Halmashauri ambazo kamati imekwisha kutembelea na thamani ya fedha kutokuonekana kwenye miradi yao, hivyo amezitaka Halmashauri zote kusimamia thamani ya fedha katika miradi yao.
Mhe. Nyamoga ameyasema hayo katika Ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya afya, na miundombinu ya Barabara inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging`ombe Mkoani Njombe ikiwiwa ni mwendelezo wa Ziara ya Kamati hiyo ya siku tatu Mkoani hapo.
Aidha kamati imeielekeza Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri kufikilia njia mbadala ya kuweka Uzio katika Hospitali ya Wilaya ya Wanging`ombe kwa lengo la kuboresha ulinzi na usalama wa wananchi wote watakaokuwa wakipatiwa huduma katika hospitali hiyo.
Katika hatua nyingine Wajumbe wa Kamati hiyo wameishauri Halmashauri kupanda miti ya matunda na vivuli katika Zahanati, vituo vya afya na hospital ya Wilaya ili kuendeleza utunzaji wa mazingira na pia kutumika kama maeneo ya kupumzika kwa wananchi wanaopatiwa huduma katika viyuo hivyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali imeyapokea yote yaliotolewa na kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Kwenda kuyatekeleza.