Featured Kitaifa

MAMA NA MWANA WAFANYIWA UNYAMA DODOMA

Written by mzalendo

Na Gideon Gregory, Dodoma.

Mwanamke mmoja mkazi wa Mtaa wa Muungano A kata ya Mkonze Jijini Dodoma aitwaye Mwanvita Mwakibasi (33) amepoteza maisha pamoja na mtoto wake Salma Silvester (13) kwa kile kinachodaiwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya shingoni na mgongoni na kuingiliwa kinyume na maumbile na watu wasiojulikana.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa mtoto mkubwa wa marehemu (jina limehifadhiwa) amesema ilipofika muda wa saa 9 usiku mdogo wake alimfata chumbani na kumwambia haamke akamuone mama yao anatokwa na damu kitandani.

“Baada ya hapo nilitoka nankwenda sebleni nikakuta mlango wa chumbani kwa mama ukowazi nikapita nikaingia ndani ndipo nikachukua simu nikampigia bibi japo mama mkubwa ni jirani yetu ila sikuwa na namba yake ndipo nikampigia ilinaweze kumpigia aje ndipo akampigia na akaja”,amesema.

Amesema baada ya mama yake mdogo kufika na majirani ndipo walipomchukua na mdogo wake hospitali.

Kwa upande wake dada wa marehemu Pendo Mwanvita amesema ilikuwa mishale ya saa Nane usiku alipigiwa simu na mama yake kutoka Mbeya kuwa haende kumuangalia mdogo wake kavamiwa na majambazi kuwa kapigiwq simu na mjukuu wake wa kiume mwenye umri wa miaka 14.

“Huyo hiyo siku alilala na watoto wake wawili kitandani wakike wawili na yeye hasa mdogo alihamka kwenda uhani akamuamsha mama yake, mama nipelek uhani lakini baada ya kuhamka akaona mama yake ametapakaa damu ndipo ikabidi amuamshe kaka yake akatafuta simu ya mama yake hakuiona ilabidi atafute simu ampigie bibi yake aliyeko Mbeya kwani ndiyo namaba ya simu aliyoshika kichwani”,amesema.

Amesema alipofika alimkuta Mwanvita amelala ndipo akaita majirani wakampeleka hospitali na kuongeza kuwa hospitali walikwenda na polisi na kurudi nao nyumbani kwaajili ya kufanya uchunguzi wa tukio hilo ndipo wakapata taarifa kuwa tiyari mmoja kashafariki japo mwingime yupo katima hali mbaya na kuja kufariki baadae wakati akipatiwa matibabu.

Naye Mwenyekiti wa mtaa huo Yona Wami amesema tukio hilo limewashtua sana kutoka na hali ilivyokuwa kwani hawajazoea kutokea matukio ya aina hiyo katika maeneo yao na wamekuwakuwa wakiyasikia katika sehemu zingine yakitokea tofauti na ilivyo sasa.

“Kwanza nashangaa na nasikitika kwann imetokea hivi yaani hili tukio limetupa hofu kubwa kwasababu matukio ya namna hii sisi hayajawahi kutokea hapa halafu leo hii watu wawili kwa mpigo hii haikubaliki hata kidogo lazima uchunguzi ufanyike juu ya tukio kama hili.

Kaiumu mkuu wa kitengo Cha mawasiliano na uhusiano katika hospital ya rufaa mkoa wa Dodoma Genero Lazalo Mbise amethibitisha kupokea mwili mmoja wa marehemu pamoja na majeruhi mmoja ambaye ni mtoto ambaye baadae naye alipoteza maisha wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Jitihada za kulitafuta jeshi la polisi Mkoa wa Dodoma kuthibitisha tukio hilo zinaendelea baada ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo SACP George Katabazi kusema yupo kwenye kikao na atazungumza mara ya baada ya kutoka kikaoni.

About the author

mzalendo