Featured Kimataifa

DKT. TULIA AWASILI NCHINI ITALIA

Written by mzalendo

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 5 Septemba, 2024 amewasili Verona, nchini Italia ambako anatarajia kushiriki katika Mkutano wa 22 wa Maspika wa Mabunge ya nchi za G7, unaotarajiwa kufanyika nchini humo kuanzia tarehe 5 hadi 8 Septemba, 2024.

Mhe. Dkt. Tulia ataiwakilisha IPU katika Mkutano huo ambapo ujumbe mkuu atakaouwasilisha ni umuhimu wa ushirikiano wa Kimataifa miongoni mwa nchi zote duniani katika kutekeleza na kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu kwa pamoja.

About the author

mzalendo