Featured Kitaifa

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA TUME NA WADAU

Written by mzalendo
Mwenyekiti
Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele,
akizungumza wakati akifungua  mafunzo ya siku
mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa
Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na
Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo
Agosti 26 hadi 27, 2024 Mkoani Mkoani Mara.
Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akizungumza wakati akifungua  mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo  Agosti 26 hadi 27, 2024 Mkoani Mkoani Mara.

**************

Na Waandishi Wetu
Watendaji wa uchaguzi katika mikoa ya Mara,
Simiyu na Manyara wametakiwa kutoa ushirikiano kwa Tume Huru ya Taifa ya
Uchaguzi na wadau wa uchaguzi wakati wa kutekeleza majukumu yao ili kufanikisha
zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mikoa yao.

Wito huo umetolewa leo tarehe 26 Agosti, 2024
na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe.
Jacobs Mwambegele wakati akifungua mafunzo ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu
la Wapiga Kura kwa watendaji wa uboreshaji ngazi ya mkoa na halmashauri
yaliyofanyika katika mji wa Musoma mkoani Mara.

Jaji Mwambegele amesisitiza kuwa ni muhimu
kwa watendaji hao kuhakikisha kuwa wanafuata maelekezo ya Tume na kushirikiana
kikamilifu ili kuhakikisha zoezi la uboreshaji linaenda vizuri na kwa ufanisi.
“Ninawasihi muwe na ushirikiano mzuri na wa
karibu na Tume wakati wote mtakapokuwa mnatekeleza majukumu yenu na ikiwa
mnahitaji ufafanuzi au maelekezo yoyote, msisite kuwasiliana na Tume,” amesema
Jaji Mwambegele.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa
ya Uchaguzi Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk
ambaye alifungua mafunzo kama hayo mkoani Simiyu amewataka watendaji hao kutoa
ushirikiano kwa mawakala wa vyama vya siasa, asasi za kutoa elimu ya mpiga kura
na waangalizi wa zoezi hilo.

Mkoani Manyara, mafunzo kwa watendaji wa
uchaguzi ngazi ya mkoa yalifunguliwa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Asina Omari ambaye amewataka watendaji hao
kuzingatia mafunzo hayo ili waweze kuwafundisha Maafisa waandikishaji wasaidizi
ngazi ya kata.

“Mafunzo haya yanawajengea umahiri wa
kuwafundisha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata ili nao wakatoe
mafunzo hayo kwa waendeshaji wa vifaa vya Bayometriki na Waandishi wasaidizi
ambao ndiyo watakaohusika na uandikishaji wa wapiga kura vituoni,” amesisitiza
Jaji Asina.

Kufanyika kwa mafunzo hayo, ni maandalizi ya
kuanza kwa mzunguko wa nne wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
ambao unajumuisha mkoa wa Mara, Simiyu na
baadhi ya halmashauri za Mkoa wa Manyara ambazo ni Halmashauri ya Mji wa
Babati na Halmashauri za Wilaya za Babati, Hanang na Mbulu ambapo uboreshaji
utaanza tarehe 04 Septemba, 2024 hadi 10 Septemba, 2024 na vituo vitakuwa
vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

Makamu Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji wa Rufaa(Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk, akizungumza wakati akifungua  mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo  Agosti 26 hadi 27, 2024 Mkoani Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Selemani Mtibora akizungumza wakati wa mafunzo hayo mkoani Simiyu.

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari  akizungumza wakati akifungua  mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo  Agosti 26 hadi 27, 2024 Mkoani Mkoani Manyara.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi. Giviness Aswile  akizungumza jambo wakati wa Mafunzo hayo mkoani Manyara. 

Washiriki wa Mafunzo yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)  kwa Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Simiyu, wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kutunza siri wakati wa kutekeleza majukumu yao . Mafunzo hayo yameanza leo Agosti 26, 2024 na yamehusisha Mratibu wa Mkoa wa Uboreshaji wa Daftari, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Uchaguzi, Maafisa TEHAMA na Maafisa Ugavi wa halmashauri zote za mkoa wa Simiyu.

 

Washiriki wa Mafunzo yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)  kwa Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Manyara, wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kutunza siri wakati wa kutekeleza majukumu yao . Mafunzo hayo yameanza leo Agosti 26, 2024 na yamehusisha Mratibu wa Mkoa wa Uboreshaji wa Daftari, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Uchaguzi, Maafisa TEHAMA na Maafisa Ugavi wa halmashauri zote za mkoa wa Manyara.

Washiriki wa Mafunzo yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)  kwa Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Manyara, wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kutunza siri wakati wa kutekeleza majukumu yao . Mafunzo hayo yameanza leo Agosti 26, 2024 na yamehusisha Mratibu wa Mkoa wa Uboreshaji wa Daftari, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Uchaguzi, Maafisa TEHAMA na Maafisa Ugavi wa halmashauri zote za mkoa wa Manyara.

Washiriki
wa Mafunzo yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)  kwa
Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Mara, wakila
kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kutunza siri wakati wa
kutekeleza majukumu yao mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya
Musoma,Bi.  Aristida Tarimo. Mafunzo hayo
yameanza leo Agosti 26, 2024 na yamehusisha Mratibu wa Mkoa wa Uboreshaji wa
Daftari, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Uchaguzi, Maafisa TEHAMA na Maafisa
Ugavi wa halmashauri zote za mkoa wa Mara.

Washiriki
wa Mafunzo yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)  kwa
Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Mara, wakila
kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kutunza siri wakati wa
kutekeleza majukumu yao mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya
Musoma,Bi.  Aristida Tarimo. Mafunzo hayo
yameanza leo Agosti 26, 2024 na yamehusisha Mratibu wa Mkoa wa Uboreshaji wa
Daftari, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Uchaguzi, Maafisa TEHAMA na Maafisa
Ugavi wa halmashauri zote za mkoa wa Mara.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Musoma,Bi.  Aristida Tarimo akitoa maelekezo kabla ya kuwaapisha. 

About the author

mzalendo