Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL ni miongoni wa Wadau wanaoshiriki katika maonesho ya 31 ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nanenane Nzuguni, jijini Dodoma kuanzia tarehe Agosti 1 hadi Agosti 8,2024.
Shirika hilo linashiriki kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanaotembelea maonesho ya Nanenane wanapata elimu kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na Shirika ambazo zinasaidia katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali kama kilimo na nyinginezo.
“Tumekuja kushiriki katika maonesho haya ya Nanenane na tumeleta huduma nyingi ikiwemo Tpesa itakayowezesha wateja kutoa na kutuma pesa,wateja watasajili laini na watapata elimu namna ya kutunza data zao Kimtandao katika kituo chetu mahiri cha NIDC na huduma nyingi hivyo tunawakaribisha sana bandani kwetu” Amesema Afisa Uhusiano wa TTCL Bi.Ester Mbanguka.
Mbali na huduma zingine katika banda la TTCL wanatoa huduma ya malipo ya Mkupuo kwa Vibarua ambayo yanarahisisha katika ulipaji wa Vibarua ambayo ni ya Kidijitali.
Ikumbukwe kuwa maonesho haya ya Kilimo ya Kimataifa Nane Nane kwa mwaka 2024, yenye Kauli mbiu isemayo “Chagua viongozi bora wa Serikali za mitaa kwa maendeleo endelevu ya Kilimo, mifugo na Utaliiā yalizinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) na yatafikia kilele chake ni Agosti 8 Mwaka huu.
#IshiKidijitali
#Nanenane2024