Featured Kimataifa

MKUU WA JESHI LA SUDAN ANUSURIKA KATIKA JARIBIO LA MAUAJI

Written by mzalendo

Jeshi la Sudan limetangaza kuwa kamanda wake mkuu, Jenerali Abdel-Fattah al Burhan amenusurika katika shambulio la ndege mbili sisizo na rubani (droni) katika hafla ya wahitimu wa jeshi ambapo katika shambulio hilo Watu watano wameuawa.

Jeshi la Sudan limeeleza katika taarifa yake kuwa shambulio hilo la droni mbili limetokea katika mji wa Gebeit wa mashariki mwa Sudan baada ya kumalizika hafla hiyo ya wahitimu wa mafunzo ya jeshi,
Kamanda wa jeshi la Sudan, Jenerali Abdel-Fattah al Burhan hakudhurika katika hujuma hiyo ya droni.

Sudan imeathiriwa na vita kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa kati ya jeshi la nchi hiyo na kundi la wanapiganaji lenye nguvu liitwalo Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) linaloongozwa na Jenerali Hamdan Dagalo.

Chanzo cha habari Pars Today.

About the author

mzalendo