Featured Kitaifa

NIDA YATOA UFAFANUZI KASORO VITAMBULISHO

Written by mzalendo

MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imesema kuwa
vitambulisho vinavyotolewa na NIDA vina ubora unakidhi viwango vya kimataifa na kwamba wataalam wanaendelea na uchunguzi wa kubaini chanzo cha tatizo lilikuwa ni nini.

Pia inatoa rai pia kwa watendaji wa serikali za kata, mitaa, vijiji, vitongoji na shehia kwa upande wa Zanzibar, kuvikusanya vitambulisho hivi na kuvirejesha kwenye ofisi zetu za NIDA wilayani ili viweze kuchapishwa upya bila malipo yeyote kwa mwananchi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Julai 222024 Mkurugenzi wa Idara ya Vitambulisho kutoka NIDA Edson Guyai wakati akitoa ufafanizi kuhusu kuwapo kwa baadhi Vitambulisho hivyo kufutika
amesema kumekuwa na upotoshaji mkubwa kuhusu ubora wa vitambulisho vya Taifa kutokana na changamoto hiyo ndogo iliyojitokeza.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa wamepokea taarifa ya kuwepo kwa Vitambulisho vichache kufutika (Taarifa zailizochapwa mbele au nyuma ya kitambulisho mfano majina, au Namba ya Kitambulisho au tarehe ya kuzaliwa.

“Katika kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto ya wananchi wengi kutokuwa na vitambulisho vya Taifa Serikali ya awamu ya Sita iliwezesha fedha kiasi cha Biloni 42.5 kwa ajili ya ununuzi wa kadighafi,” amesema.

Amefafanua kuwa baada ya kuwezeshwa NIDA ilipanga na kutekeleza Mkakati wa Uzalishaji Vitambulisho mkubwa (Mass production) ulikwenda sambamba na Usambazaji na Ugawaji mkubwa wa Vitambulisho kwa umma (Mass Distribution and Mass Issuence).

Amesema kuwa tayari umekwisha zalisha vitambulisho takribani vya watu wote waliokuwa NIN kwa muda mrefu na kuvipeleka huko kwenye ofisi nilizozitaja ambapo bado kuna vitambulisho vingi havijachukuliwa na kwambia wananchi waende wakachukue vitambulisho vyao.

Amesema jumla ya Vitambulisho milioni 21 kwa watu wote wenye sifa vimezalishwa na kupelekwa katika ngazi ya Mtaa, vijiji, Kata,na Shehia.

Ameongeza kuwa jumla ya Vitambulisho million 19 zimechukuliwa na wananchi.

About the author

mzalendo