Featured Kitaifa

JAMII YAASWA KUENZI MILA YA UNYAGO ILI KULINDA MAADILI

Written by mzalendo
Mkufunzi Dkt. Lovemore Mazibuko (kushoto) akimsikiliza mmoja wa washiriki aliyekuwa akitoa ufafanuzi wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa utamaduni kuhusu namna ya kuandaa orodha ya kitaifa ya urithi wa utamaduni usioshikika yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yaliyowakutanisha wataalamu kutoka wizara za Utamaduni na Sanaa Tanzania Bara na Visiwani na wa Sekta binafsi mjini Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Mwali akiwa amelala miguuni mwa kungwi wakati wa sherehe za unyago zilizofanyika mwishoni mwa wiki wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani.

Mkufunzi Dkt. Lovemore Mazibuko akiwasilisha mada kwa wadau wa utamaduni wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa namna ya kuandaa orodha ya kitaifa ya urithi wa utamaduni usioshikika yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) mjini Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. Wadau hao ni wataalamu wa masuala ya utamaduni kutoka Tanzania Bara na Visiwani na wa Sekta binafsi mjini Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Wadau wa utamaduni na Sanaa wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na mkufunzi Dkt. Lovemore Mazibuko kutoka Malawi wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa namna ya kuandaa orodha ya kitaifa ya urithi wa utamaduni usioshikika yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kukutanisha wataalamu kutoka wizara zote za Tanzania Bara na Visiwani na wa Sekta binafsi mjini Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Mkufunzi Dkt. Maximilian Chami akiwasilisha mada kwa washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa utamaduni ambao ni watalamu kutoka Tanzania Bara na Visiwani kuhusu namna ya kuandaa orodha ya kitaifa ya urithi wa utamaduni usioshikika yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) mjini Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Mmoja wa washiriki Philomena Mwalongo akiwasilisha mada ya kundi lake wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa utamaduni ambao ni wataalamu wa masuala ya utamaduni kutoka Tanzania Bara na Visiwani kuhusu namna ya kuandaa orodha ya kitaifa ya urithi wa utamaduni usioshikika yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) mjini Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Mmoja wa washiriki Philip Maligisu akiwasilisha mada ya kundi lake wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa utamaduni ambao ni wataalamu wa masuala ya utamaduni kutoka Tanzania Bara na Visiwani kuhusu namna ya kuandaa orodha ya kitaifa ya urithi wa utamaduni usioshikika yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) mjini Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Wadau wa utamaduni wakijadiliana wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa namna ya kuandaa orodha ya kitaifa ya urithi wa utamaduni usioshikika yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Wadau hao ni watalaamu wa masuala ya utamaduni Tanzania Bara na Visiwani na wa Sekta binafsi mjini Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Wadau wa utamaduni wakijadiliana wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa namna ya kuandaa orodha ya kitaifa ya urithi wa utamaduni usioshikika yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Wadau hao ni watalaamu wa masuala ya utamaduni Tanzania Bara na Visiwani na wa Sekta binafsi mjini Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
 
Wadau wa utamaduni wakijadiliana wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa namna ya kuandaa orodha ya kitaifa ya urithi wa utamaduni usioshikika yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Wadau hao ni watalaamu wa masuala ya utamaduni Tanzania Bara na Visiwani na wa Sekta binafsi mjini Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Washiriki wa mafunzo ya kujenga uwezo wa kuorodhesha na kuuhifadhi utamaduni usioshikika wakiwa kwenye picha ya pamoja mjini Bagamoyo. Mafunzo hayo yaliandaliwa na UNESCO
 
Na Mwandishi wetu – Bagamoyo
 
Jamii imeaswa kuendelea kuzienzi mila na desturi za kitanzania kama Unyago kwa wasichana ili kukabiliana na mmonyoko wa maadili nchini Tanzania.
 
Wito huu ulitolewa hivi karibuni mjini Bagamoyo na Nyakanga Pili wakati wa ziara ya mafunzo kwa vitendo iliyoandaliwa na shirika la UNESCO kama moja ya mikakati ya kushirikisha jamii ili kuhifadhi utamaduni usioshikika.
 
Nyakanga, ni jina linalotumika kwa walimu wa Mwali, binti anaefundwa katika Jamii ya Wakwere na Wadoe wilayani bagamoyo, mkoa wa Pwani.
 
Nyakanga Pili alisisitiza kwamba mafunzo ya Unyago yamekuwa yakibadilika kutokana na Maendeleo ya elimu ambapo kwa sasa hutolewa katika umri wa kuanzia miaka 18 na mara nyingi wakati wa likizo za shule.
 
“ Wakati wa Unyago tunawafunda mabinti wawe wasafi, wawe na adabu na wasiwe waongo. Tunawafunza nidhamu na kusisitiza kuheshimu wakubwa,” alisema.
 
Alisisitiza kuwa kuiga mambo ya wazungu kumefanya jamii hususani kizazi cha sasa kuwa na vijana ambao hawaheshimu wakubwa na kuongezeka kwa mmonyoko wa maadili kwenye kjamii,
 
Kwa upande wake, wakili Philomena Mwalongo ambae ni Mkurugenzi wa YOGE alisisitiza umuhimu wa kutengeneza maktaba ya utamaduni wa urithi usioshikika ili kuweza kurithisha mila na desturi kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
 
Mafunzo hayo yalihusisha mafunzo kwa vitendo ambapo washiriki walikwenda kujifunza namna ya kuhifadhi vyakula kwa njia za asili, kupika vyakula vya kiasili na ngoma ya Vanga na kuangazia ni namna gani ujuzi huu unarithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

About the author

mzalendo