Featured Kitaifa

KIKUNDI CHA WOMANKIND INITIATIVE CHAPATA MSAADA KUTOKA NVeP KWA UFADHILI WA BARRICK

Written by mzalendoeditor
Kaimu Meneja Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Victor Lule,(wa tatu kutoka kushoto) akimkabidhi Mfano wa Hundi ya Dola $ 10,0000 Mwakilishi wa kikundi cha Womankind Initiative Christina Samwel katika hafla hiyo .Wengine pichani ni wafanyakazi wa mgodi huo.

 
Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Victor Lule akimkabidhi Mfano wa Hundi ya Dola $ 10,0000 Mwakilishi wa kikundi cha Womankind Initiative Christina Samwel katika hafla hiyo .Wengine pichani ni wafanyakazi wa mgodi huo
Mwakilishi wa kikundi cha Womankind Initiative, Christina Samweli (katikati) akiwa na wafanyakazi wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu katika hafla hiyo iliyofanyika katika mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP), kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick, imetoa msaada wa dola za Kimarekani 10,000 kwa Shirika lisilo la Kiserikali la WomanKind Initiative, lililopo Kahama mkoani Shinyanga kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za athari za mabadiliko ya tabia nchi zinazolenga kupunguza wimbi la umaskini kwa Wanawake na Watoto.

 

Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, kwa ajili ya kusaidia makundi maalum kama vile Wanawake, watoto na makundi mengine yenye uhitaji yasiofaidika na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.
Kila robo ya mwaka taasisi ya NVeP imeweza imeweza kutoa misaada yenye tija na manufaa ya moja kwa moja kwenye jamii zenye uhitaji barani Afrika na kufikia sasa zaidi ya mashirika 20 yasiyo ya Kiserikali na taasisi za kijamii nchini yamepatiwa msaada huo na tayari umeleta mabadiliko chanya katika jamii hususani katika sekta ya elimu, afya kwa Wanawake na watoto na utunzaji wa Mazingira.
Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi huo, Victor Lule, alisema NVeP, itaendelea kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanatoa huduma kwa jamii kwendana na malengo ya taasisi hiyo sambamba na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
“Tunajivunia kuona fedha zinazotolewa na Barrick kwa kushirikiana na NVeP zinasaidia kuleta mabadiliko chanya katika jamii kwenye maeneo mbalimbali nchini na tunaamini shirika la Women Kind, nanyi mtatumia fedha hizi kwa lengo lililokusudiwa” ,alisema Lule.
Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la WomanKind, Christina Samweli , ambaye alipokea hundi kwa niaba ya taasisi hiyo , alishukuru kupatiwa msaada huo na alisema kuwa utasaidia kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.

 

About the author

mzalendoeditor