MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele ,akiangalia bidhaa zinazozalishwa na JKT katika banda la JKT kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biasharayoendelea jijini Dodoma.
Na.Mwandishi Wetu
MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini nakuifanya Tanzania kuwa mahali salama pa kufanya biashara na uwekezaji.
Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la JKT kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ,Meja Jenerali Mabele amesema hali hiyo imefanya watu wengi zaidi kuja kuwekeza hapa nchini.
“Naipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira ya mazuri ya kufanya biashara na hivyo watu wengi zaidi kuja kuwekeza hapa nchini na hivyo kuifanya Tanzania kuwa mahali sahihi pa kufanya biashara na uwekezaji.
Meja Jenerali Mabele ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la uzalishaji Mali la JKT (SUMAJKT) amesema wameshashiriki maonesho hayo mara nyingi na kwamba wamekuwa wakija na bidhaa bora ili wananchi wapate bidhaa bora.
Pia amesema SUMAJKT ina kampuni bora ya ulinzi ambayo imeajiri vijana wa Kitanzania zaidi ya 16000 na
kupunguza ombwe la ajira nchini.
“Maonesho haya sisi tunafanya biashara ambayo husaidia kuongeza uchumi wa nchi, na mwezi wa sita mwaka huu ,tumeshiriki katika kutoa gawio kwa hiyo ni wachangiaji katika mfuko mkuu wa Serikali, tunalipa kodi ,tena ni walipa kodi wazuri katika nchi yetu,hivi vifaa vyote mnavyoviona hapa tunalipa kodi na hili ni jambo la msingi sana.
Kuhusu ushiriki wao amesema,wamekuwa wakishiriki maonesho hadi ya nje ya nchi na wameshaenda kwenye maonesho Commoro ambapo wakati mwingine watu wa Comoro wanakuja kuzifuata bidhaa za SUMAJKT Dar es Saaam .
Brigedia Jenerali Hassan Mabena Mkuu wa Tawi la Utawala JKT amesema JKT wanashiriki maonesho hayo ambapo malengo yao ambayo ni malezi ya vijana uzalishaji mali na ulinzi wa Taifa .
“JKT limekuwa likifanya shughuli za uzalishaji mali katika Nyanja za kilimo na uvuvi na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali pamoja na shirika letu la uzalishaji mali (SUMAJKT),
“Kwa kuwa JKT limekuwa likichukua vijana wale wa kujitolea na wale wa mujibu wa sheria,pamoja na kufundishwa masomo ya ukakamavu ,uzalendo na hali ya kulipenda Taifa lao lakini vile vile wamekuwa wakifudishwa katika Nyanja za uzalishaji mali
‘katika eneo hilo vijana wamefundishwa kuzalisha bidhaa mbalimbali na kupitia vikosi na shirika lao vijana kutumia maeneo hayo kama shamba darasa.
Ameshukuru kwa uwepo wa maonesho haya kwani yamekua yakichangia katika kuwafundisha vijana kwa nadharia na vitendo.