Featured Kitaifa

WADAU WAKUTANA KUJADILI UTEKELEZAJI MALENGO YA SDGs

Written by mzalendo
NAIBU  Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Dkt. Lorah Madete,akizungumza wakati akifungua  Warsha ya Jukwaa la  kitaifa ya kuimarisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) lililowashirikisha wadau kutoka Serikalini na asasi za kiraia lililofanyika leo Juni 28,2024 jijini Dodoma.
 
Mchumi Mwandamizi kutoka Ofisi a Rais – Tamisemi.  Idara ya Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bi. Stella Saasita ,akizungumza wakati wa Warsha ya Jukwaa la  kitaifa ya kuimarisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) lililowashirikisha wadau kutoka Serikalini na asasi za kiraia lililofanyika leo Juni 28,2024 jijini Dodoma.
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Salome Makamba,akizungumza wakati wa Warsha ya Jukwaa la  kitaifa ya kuimarisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) lililowashirikisha wadau kutoka Serikalini na asasi za kiraia lililofanyika leo Juni 28,2024 jijini Dodoma.
MBUNGE wa Kasulu Vijijini, Mhe.Augustine Vuma ,akizungumza wakati wa Warsha ya Jukwaa la  kitaifa ya kuimarisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) lililowashirikisha wadau kutoka Serikalini na asasi za kiraia lililofanyika leo Juni 28,2024 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Dkt. Lorah Madete,(hayupo pichani)  wakati akifungua  Warsha ya Jukwaa la  kitaifa ya kuimarisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) lililowashirikisha wadau kutoka Serikalini na asasi za kiraia lililofanyika leo Juni 28,2024 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
NAIBU  Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Dkt. Lorah Madete amefungua Warsha ya kitaifa ya kuimarisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyowashirikisha wadau kutoka Serikalini na asasi za kiraia ili kujadili changamoto zinazoleta vikwazo kwa utekelezwaji wa Malengo ya SDGs kwa wakati.
Akizungumza na waandishi wa habari  mara baada ya kufungua Warsha ya Jukwaa la Taifa la Kuimarisha utekelezaji wa malengo ya SDGs iliyofanyika leo Juni 28,2024 jijini Dodoma.
Dkt.Madete amesema kuwa mchango wa wadau ni muhimu katika utekelezaji wa mpango huo.
‘Kama nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, mnamo Septemba 2015, tulipitisha Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu ambayo, pamoja na mambo mengine, ilibainisha malengo 17 na 169 yaliyoundwa ili kukabiliana na changamoto kubwa zaidi duniani,’ amesema Dkt.Madete
Aidha amezitaja changamoto hizo kuwa ni  kutokomeza umaskini na njaa.,kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na kukuza amani na haki.
“Ajenda hii pana inatumika kama mwongozo wa kuongoza nchi kuelekea maendeleo endelevu, kuhakikisha kwamba ukuaji wa uchumi, ushirikishwaji wa kijamii, na ulinzi wa mazingira unafikiwa kwa maelewano na Dunia ifikapo 2030,’ amesema
Amesema  kuwa Tanzania ilichagua kutekeleza ajenda hiyo pamoja na mipango na mikakati ya kisekta. “Kwa bahati nzuri kwa Tanzania, mchakato wa kupitishwa kwa SDGs ulienda sambamba na utayarishaji wa mifumo ya maendeleo ya muda wa kati nchini (Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 – unaojulikana kwa ufupi kama FYDP II,” 
Hata hivyo ameeleza  kuwa mkutano huo utajadili  mikakati ya kuimarisha mifumo ya data na michakato ya ufuatiliaji, kutokana na maarifa kutoka kwa ripoti ya tathmini ya pengo la data ya Tanzania SDGs, ili kufuatilia kwa ufanisi maendeleo Pia kujadi  mbinu bunifu za kuhamasisha rasilimali na kufadhili mipango ya SDG, kama ilivyo  katika ripoti ya ukaguzi wa ufanisi wa utekelezaji wa SDG.
Kwa upande wake Mchumi Mwandamizi kutoka Ofisi a Rais – Tamisemi.  Idara ya Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bi. Stella Saasita amesema  kuwa Tamisemi wanatafsiri SGD’s pale wananchi wanapopata huduma hospitali na wakulima wapate pembejeo na mbegu 
“Wananchi wanapoguswa na huduma mbalimbali zinazotolewa ni utekelezaji wa moja kwa Moja wa malengo,” amesema 
Naye  Mratibu wa Jukwaa La Maendeleo Endelevu Tanzania, Stephen Chacha amesema kuwa wanaangalia namna ya kutekeleza mipango ya kikanda
Aidha amesema kuwa wanashirikiana na Serikali katika kuandaa mipango ya Maendeleo ya Kitaifa, mchakato ya sera za Kitaifa na wamepewa wigo Wa Kuandaa ripoti za  kitaifa..

About the author

mzalendo