Featured Kitaifa

SERIKALI YARIDHIA MIKATABA 12 YA MAZINGIRA

Written by mzalendo

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu maswali bungeni wakati wa Kikao cha 45 Mkutano wa 15 wa Bunge jijini Dodoma leo Juni 10, 2024.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba wakati wa Kikao cha 45 Mkutano wa 15 wa Bunge jijini Dodoma leo Juni 10, 2024.

……

Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imeridhia mikataba ya Ofisi ya Makamu wa Rais imeridhia mikataba 12 ya kimataifa na kikanda kuhusu Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ameliarifu Bunge wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Maryam Azan Mwinyi aliyetaka kujua mikataba mingapi ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi ambayo watumishi wake wanatoka Zanzibar.

 

Akiendelea kujibu swali hilo Mhe. Khamis amesema utekelezaji wa mikataba hiyo hufanyika kwa ushirikiano na uratibu baina ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania Zanzibar.

 

Kutokana na ushirikiano huo, amesema utekelezaji wa mikataba hiyo hujumuisha watumishi wote wa pande zote mbili za Muungano akifafanua kuwa Ofisi hizo mbili zimekuwa zikishiriki kwa pamoja kwenye vikao vya maamuzi vya mikataba hii. 

 

Halikadhalika, Naibu Waziri Khamis amebainisha kuwa pande zote mbili za Muungano zinanufaika na utekelezajiwa mikataba hii hususani kupitia, programu na miradi inayoratibiwa kupitia Mikataba hii.

 

Hivyo, amesema Tanzania Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kusimamia utekelezaji wa Mikataba ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi kwa maslahi mapana ya Taifa ili kukabiliana na changamoto za kimazingira na athari za mabadiliko ya tabianchi.

About the author

mzalendo