Featured Kitaifa

WANANCHI WASHAURIWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUWEKA AKIBA YA FEDHA

Written by mzalendo

Afisa Usimamizi wa Fedha katika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha – Wizara ya Fedha, Bw.Stanley Kibakaya, akitoa elimu ya fedha kwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Afisa Tabibu Kibondo, mkoani Kigoma.

Na. Chedaiwe Msuya,WF, Kigoma

Wananchi wametakiwa kukopa mikopo yenye faida kwenye taasisi au mtu binafsi ambaye ana leseni iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania ili kuwa na uhakika wa mkopo na kuondoa changamoto kwa wananchi hao.

Wito huo umetolewa katika Kata ya Mabamba, Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma na Afisa Usimamizi wa Fedha katika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha katika Wizara ya Fedha Bw. Stanley Kibakaya, wakati wa zoezi la kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali katika Mkoa wa Kigoma.

“Hakikisha unapokwenda kukopa, mkopeshaji awe na leseni kwa kuwa mtoa huduma huyo atakuwa amekidhi vigezo na masharti vilivyowekwa na mamlaka husika”, alisema Bw. Kibakaya.

Aidha, aliwahimiza wafanyabiashara kuwa na utamaduni wa kuweka akiba ili kuweza kutambua mapato wanayo yapata kupitia biashara zao

Alisema kuwa wakitunza fedha lazima wawe na malengo ili akiba hiyo iwe na faida na pia ni vema wahifadhi fedha kwenye akaunti za Benki au kwenye simu,  sehemu ambazo ni salama ili kuepuka hasara au upotevu.

Kuhusu uwekezaji, Bw. Kibakaya, alisema kuwa   jambo hilo si kwa ajili ya watu wenye kampuni kubwa pekee bali hata mwananchi wa kawaida anaweza kuwekeza kupitia biashara ndogondogo anazozifanya.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mabamba, Wilayani Kibondo Bw. Shedrack Chongela, aliipongeza Wizara ya Fedha kwa elimu waliyoitoa kwa wananchi hao huku akiwakumbusha wananchi wanapokwenda kuchukuwa mikopo waende maeneo yenye kukidhi vigezo.

Naye Mkazi wa Kijiji cha Mabamba, Wilaya ya Kibondo, Bi. Felister Kazombe, alisema kuwa semina hiyo ni muhimu kwa jamii yao kwa kuwa imetoa mwongozo mzuri kuhusu masuala ya fedha.

Diwani wa Kata ya Mabamba, Wilaya ya Kibondo, Mhe. Shedrack Chongela, akizungumza na wananchi kuhusu mafunzo ya Elimu ya Fedha na Uwekezaji yaliyofanyika katika Soko la Mabamba Wilaya ya Kibondo, Kigoma.

Afisa Usimamizi wa Fedha katika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha katika Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, akitoa semina ya mafunzo ya Elimu ya Fedha na Uwekezaji kwa wanafunzi wa Chuo cha Afisa Tabibu Kibondo, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho kilichopo kata ya Kibondo mkoani Kigoma.

Afisa Usimamizi wa Fedha katika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha katika Wizara ya Fedha, Bi. Grace Samwel akitoa semina kuhusu Elimu ya Fedha na Uwekezaji kwa wanafunzi wa Chuo cha Afisa Tabibu Kibondo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo mkoani Kigoma.

Baadhi ya Wajasiriamali wakisikiliza semina kuhusu Elimu ya fedha na uwekezaji yaliyofanyika katika soko la Mabamba, Wilaya ya Kibondo.

Afisa Usimamizi wa Fedha katika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha – Wizara ya Fedha Bi. Grace Samwel, akitoa elimu ya fedha kwa Wajasiriamali katika soko la Mabamba, Wilaya ya Kibondo.

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Afisa Tabibu Kibondo wakisikiliza semina ya Elimu ya Fedha na Uwekezaji yaliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho, Mkoani Kigoma.

Afisa Usimamizi wa Fedha katika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha – Wizara ya Fedha, Bw.Stanley Kibakaya, akitoa elimu ya fedha kwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Afisa Tabibu Kibondo, mkoani Kigoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WF, Kigoma)

About the author

mzalendo