Featured Kitaifa

Wakurugenzi dhibitini mianya ya upotevu wa mapato – Mchengerwa

Written by mzalendo

Na Mwandishi Wetu, Mikumi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka wakurugenzi wote nchini kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato ya halmashauri na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati alipotembelea Kituo cha Afya Mikumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro wakati wa ziara yake mkoani humo leo tarehe 20.05.2024.

Amesema wakurugenzi wanapaswa kuwa makini kuwasimamia maafisa biashara, wahasibu wa mapato na wataalamu wengine kwa sababu wanaweza kufanya vitu huko ambavyo hawavijui na mwisho wa siku wakawajibishwa wao.

“Tumesikia maeneo mengine ‘control number’ zinatolewa mbili mbili hivyo ni jukumu lenu kuhakikisha mnadhibiti mianya ya upotevu wa mapato,” alisema Mhe. Mchengerwa.

About the author

mzalendo