Featured Kitaifa

MHANDISI JOYCE KISAMO WA WIZARA YA NISHATI ATWAA TUZO YA KIMATAIFA YA LUCE 2024

Written by mzalendoeditor

 

Mhandisi. Joyce Kisamo akiwa mwenyefuraha baada ya kukabidhiwa TUZO ya LUCE ya mwanamke aliyefanya vizuri katika nishati, mazingira na sekta endelevu (Legacy Women Category).

 

🔴Ni
 Tuzo ya kutambua mchango wa mwanamke
aliyefanya vizuri katika nishati, mazingira na sekta endelevu
Ni tu
 
Na. Mwandishi wetu
Mtanzania Mha. Joyce Kisamo kutoka Wizara ya
Nishati amekua muafrika wa pili kutwaa tuzo ya LUCE ya mwanamke aliyefanya vizuri
katika nishati, mazingira na sekta endelevu.
 
Mnigeria Onyinye Anene-Nzelu ambaye ni Mkuu
wa Gridi Ndogo katika Ufikiaji wa Nishati nchini Nigeria, aliwahi kunyakua Tuzo
katika kundi la wanawake chipukizi 2023.
 
Joyce, ambaye ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa
Petroli kutoka Wizara ya Nishati alibuka mshindi wa shindano hilo la Tuzo za
LUCE katika kundi la Mwanamke mwenye uzoefu na aliyeacha alama na kuwashinda
wanawake wengine 15 kutoka mataifa mbalimbali ya Ulaya na Asia.
 
Zaidi ya kura 2,000 zilipigwa duniani kote
na kura 600 zilitosha kumpa ushindi Mha. Joyce ambaye alikuwa mwafrika pekee na
katika kinyang’anyiro hicho ameibuka mshindi kwa kuacha alama nyingi katika
utendaji wake wa kazi (Legacy Women Category).
 
Kwa ushindi huo Joyce ametambulika kimataifa
kuwa Mwanamke mwenye uzoefu, aliyefanyakazi na kuacha alama zenye manufaa
kiuchumi, kimazingira na kijamii katika Sekta Endelevu hususani Nishati Safi na
Endelevu.
 
Makabidhiano ya tuzo hiyo yamefanyika leo tarehe
16 Mei,2024 huko Florence nchini Italy kisha mshindi atahudhuria Mkutano wa masuala
ya Nishati Safi na Endelevu. (Flagship Conference) kuanzia tarehe 23 hadi 25
Mei, 2024 katika European University Institute.
 
Tuzo za LUCE, zimefanyika kwa mara ya pili na
linaandaliwa na mpango wa Lights on Women kwa ushirikiano na Landwärme na
Edison, linalenga kutambua na kusherehekea mchango mkubwa wa wanawake.
 
Lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kutetea
majukumu muhimu ya wanawake kuelekea matumizi bora ya nishati endelevu.

 

About the author

mzalendoeditor