Featured Kitaifa

MBUNGE NYONGO AMPONGEZA RAIS SAMIA KUMTUA MAMA NDOO KICHWANI

Written by mzalendo

MBUNGE wa Maswa Mashariki,(CCM) Mhe.Stanlaus Nyongo, akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2024/25 leo Mei 10,2024 bungeni jijini Dodoma.

……..

MBUNGE wa Maswa Mashariki,(CCM) Mhe.Stanlaus Nyongo, ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kazi  kubwa anayofanya kwa kumtua mama ndoo kichwani pamoja na kuendelea kuboresha huduma bora kwa watanzania.

Mhe.Nyongo ametoa pongezi hizo leo Mei 10,2024 bungeni jijini Dodoma wakati wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Amesema kuwa Rais amekuwa akifanya mambo makubwa katika sekta mbalimbali kwa kuendelea  kuboresha huduma za jamii kama elimu, afya, maji ambazo zinagusa watanzania wengi hasa waliopo vijijini  hivyo lazima apewe maua yake.

“Tukitizama katika miradi ya maji, mimi nimekuwa Mwenyekiti kamati ya afya, kuna fedha nyingi zinatengwa kwa ajili ya huduma za afya, na katika huduma za afya moja ya shughuli tulizoelekezwa zifanyike ni kupambana na kuzuia magonjwa mbalimbali ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza,”amesema Mhe.Nyongo

Aidha aamempongeza Rais Samia kwa  kupeleka maji vijijini ni hatua muhimu ya mapambano dhidi ya magonjwa ya kuambukiza kwakuwa zisipopelekwa kwenye miradi hiyo tatizo linalofuatia ni watu kupata magonjwa

About the author

mzalendo