Featured Kitaifa

SERIKALI YAENDELEA KUIMARSHA HUDUMA ZA MAABARA NGAZI YA MSINGI

Written by mzalendo

WAF, Dodoma

Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wafadhili wa Global Fund wametoa vifaa vya Tehama kwa Ofisi ya Rais TAMISEMI ili kusaidia kuongeza upatikanaji wa Huduma bora za maabara na afya kwa ngazi ya msingi.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Huduma za Uchunguzi na Matengenezo ya Vifaa Tiba, Dkt. Alex Magesa wakati akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya Tehama kati ya Wizara ya Afya na Ofis ya Rais TAMISEMI.

Dkt. Magesa amesema kuwa vifaa hivyo vinalenga kuongeza ufanisi wa matumizi ya mifumo ya kielektroniki ya maabara, kuongeza udhibiti wa ubora wa vipimo, utunzaji wa kumbukumbu na taarfa za sambuli pamoja na upatikanaji wa majibu kwa wakati kwa njia ya kielektroniki.

Dkt. Magesa amesema matokeo ya vifaa hivyo katika ngazi ya msingi ni wananchi kunufaika na ubora wa Huduma zitakazokuwa zinatolewa.

“Vifaa hivi vimegharimu zaidi ya Shilingi Milioni 286 ambavyo ni kompyuta za mezani 21, printa 59, UPS 68, Modemu 70 pamoja na Diski za nje 27 na vitasambazwa katika vituo 71 vilivyoainishwa kupatiwa vifaa hivi”, ameeleza Dkt. Magesa

Aidha ametoa wito kwa waganga wafawidhi wa vituo 71 watakaopokea vifaa hivyo kusimamia vifaa hivyo kufanya kazi iliyokusudiwa ili kuhakikisha vinatunzwa na kudumu kwa muda mrefu

Hata hivyo amewashukuru wafadhili wa Global fund na wadau wengine kwa kuendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha afya za watanzania zinaimarika katika ubora wenye viwango.

          

About the author

mzalendo