Featured Kimataifa

HAKUNA MTU ALIYE NA HAKI YA KUITISHIA ICC – DUJARRIC

Written by mzalendo

Maseneta wa Marekani walioitishia Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephen Dujarric ameeleza kuwa misaada inapaswa kuingia Ukanda wa Gaza bila ya kizuizi chochote na kwamba upande wowote haupaswi kutoa vitsho kwa wafanyakazi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).

Dujarric ambaye ni Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko New York kuwa wafanyakazi wa umoja huo waliopo Gaza wanendelea kutoa huduma katika maeneo yenye vita na bado wapo huko huku akiongeza kuwa, hakuna upande wowote ulio na haki ya kuwatishia wafanyakazi wa Mahakama ya Kimataifa ya  Jinai ICC. 

Maseneta 12 wa chama cha Republican nchini Marekani wameitishia ICC kuwa wataiadhibu vikali mahakama hiyo endapo itatoa waranti wa kumtia nguvuni Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu, kwa tuhuma za kuhusika na jinai za kivita katika Ukanda wa Gaza. 

Waungaji mkono wa Israel katika vyama viwili vya Democrat na Republican ndani ya Kongresi ya Marekani pia wametahadharisha kuwa endapo mahakama ya ICC itatoa hukumu dhidi ya Netanyahu na utawala wa Kizayuni basi taasisi hiyo ya sheria itakabiliwa na hatua za Marekani. 

Utawala wa Kizayuni wa Israel huku ukiungwa mkono na kupata himaya ya pande zote ya Marekani huku mashirika ya kimataifa yanayodai kutetea haki za binadamu yakiwa yamekaa kimya, kwa miezi saba sasa unaendelea kutekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya watu wasio na ulinzi wa Ukanda wa Gaza. 

About the author

mzalendo