Featured Kitaifa

CSSC YAPONGEZWA KUBORESHA HUDUMA ZA FAMASI NCHINI 

Written by mzalendoeditor

KAIMU Mganga Mkuu wa Serikali Ziada Sellah,akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma

Na.Alex Sonna_DODOMA

KAIMU Mganga Mkuu wa Serikali Ziada Sellah, amesema wakufunzi wa vyuo vya famasi nchini wanapaswa kuongeza ubunifu kwenye ufundishaji ili kuzalisha wataalamu wenye uwezo na ujuzi wa kutosha watakaosaidia kupunguza malalamiko ya wananchi kuhusu huduma mbovu zinazotolewa.

Sellah aliyasema hayo juzi jijini hapa wakati wa mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi.

Katika Mkutano huo ulioandaliwa na wadau wa famasia na Christian Social Services Commission(CSSC), alisema famasi ni moja kati ya kada muhimu sana kwenye sekta ya afya hivyo wakufunzi hawana budi kuhakikisha kuwa wanaongeza jitihada kwenye ufundishaji ili kupata wahitimu wenye viwango watakaotumika kuhudumia jamii.

Alisema kama wakufunzi watashindwa kusimamia wale wanao wafundisha basi utoaji wa huduma za famasi katika zahanati,vituo vya afya na hospitali utakuwa ni wa mashaka.

“Ukitoa mtaalamu mbovu tutakaye kunyooshea kidole ni wewe mkufunzi kada hii ya famasi ndiyo kada muhimu sana kwani inahusika na utoaji wa dawa na kama mtu atakosea kutoa dawa kwa mgonjwa anaweza kuharibu kila kitu hata kusababisha kifo kwa mgonjwa”alisema

Aidha, kutokana na umuhimu wa kada hiyo hadi sasa serikali imesajili vyuo vya famasi 106, ili kuongeza wataalamu wa Famasi nchini pamoja na kutoa ufadhili wa masomo.

“Lakini pia niwatake Wafamasia muendele kujiendeleza kimasomo kwani teknolojia na vitu vinabadilika kila siku ili muendane na mabadiliko hayo mnapaswa kusoma”alisema

Aidha  aliwapongeza mchango wa CSSC kuboresha huduma za afya nchini pamoja na ubunifu wao wa kutengeneza mifumo ya tehama itakayowasaidia sio tu wanafunzi bali hata walimu kuongeza uelewa wao wa masomo na huduma za famasi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa CSSC, Peter Maduki, alisema lengo la mradi huo ni kupanua na kuboresha huduma za afya. Pamoja na kutoa uelewa kwa jamii kuhusu maswala na sera mbalimbali za afya ili kuwezesha kuwa na taifa lenye afya bora.

Alisema mradi huo upo katika taasisi za mafunzo ya afya 106 pamoja na hospitali za mikoa, rufaa na za kikanda zipatazo 25 ikiwemo hospitali ya taifa ya Muhimbili, Mloganzila Bugando, KCMC, Dodoma, na hospitali ya rufaa ya kanda Mbeya.

Naibu Msajili wa Baraza la Famasi Tanzania, Godfrey Ngonela, alisema wanashukuru mradi huo ambao umesadia kuboresha mbinu za ufundishaji katika vyuo vya Famasi nchini.

“Kupitia mradi huu sisi Baraza tumekuwa tukishirikiana kuboresha mambo mbalimbali ikiwamo nyenzo za kufundishia, pamoja na mapitio na uboreshaji wa mitaala mipya ya mafunzo ya famasi kwa vyuo vya kati”alisema Ngonela

Awali Mkurugenzi wa huduma za Afya kutoka Christian Social Services Commission (CSSC) Dkt.Josephine Balati,ametoa shukrani kwa serikali na wadau wote wa famasi kwa ushirikiano wao katika kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini Tanzania

KAIMU Mganga Mkuu wa Serikali Ziada Sellah,akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa CSSC, Peter Maduki,akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa huduma za Afya kutoka Christian Social Services Commission (CSSC) Dkt.Josephine Balati,akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.

Mkuu wa Miradi, Ukanda wa Afrika kutoka shirika la action medeor e.v,Bi.Susanne Schmitz,akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.

Baadhi ya Washiriki wakimsikiliza Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Ziada Sellah (hayupo pichani),wakati wa mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.

KAIMU Mganga Mkuu wa Serikali Ziada Sellah,akigawa vitabu mara baada ya kuzindua zoezi la ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.

KAIMU Mganga Mkuu wa Serikali Ziada Sellah,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor